Nafasi za Kazi 10 Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

Zanzibar Full Time

The Ministry of Blue Economy and Fisheries (Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi) in Zanzibar (Tanzania) spearheads sustainable marine resource utilization. It drives economic growth by modernizing fisheries, promoting aquaculture, and empowering coastal communities to improve livelihoods, particularly for women.

The total number of job posts listed here for the Ministry of Blue Economy and Fisheries (Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi) is 10 posts in June 2026.

Job Title Posts
Afisa Uhifadhi wa Bahari Daraja la II (Marine Conservation Officer Grade II) 3
Afisa Uvuvi Daraja la II (Fisheries Officer Grade II) 3
Afisa Uhusiano Daraja la II (Public Relations Officer Grade II) 2
Afisa Uchumi wa Buluu Daraja la II (Blue Economy Officer Grade II) 1
Afisa TEHAMA Daraja la II (ICT Officer Grade II) 1
TOTAL POSTS 10

WIZARA YA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI

Vacancies: 5  |  Latest closing: Jun 16, 2026 Apply

Afisa Uhusiano Daraja la II-UNGUJA

Posts: 2  |  Closing: Jun 16, 2026 Apply  |  Period: 02/06/2026 - 16/06/2026  |  Scale: ZPSE - 10

Duties and Responsibilities

  • Kuitangaza Wizara kupitia Vyombo vya habari, vipeperushi, redio, magazeti na Makala.
  • Kupokea malalamiko kwa wadau na wananchi kwa ujumla juu ya utendaji wa Wizara.
  • Kufanya uchunguzi wa malalamiko yaliyowasilishwa kwa Wizara.
  • Kupekea wageni wa Ofisi.
  • Kuwasilisha malalamiko sehemu husika.
  • Kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka. na
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

Qualifications

Awe Mzanzibari awe na umri usiozidi miaka 46

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Uhusiano wa kimataifa na Diplomasia (International Relation and Diplomacy) au Uhusiano wa Umma (Public Relation) au Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) au Uandishi wa Habari (Journalism), au Masoko na Uhusiano wa Umma (Marketing and Public Relation) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Awe na mlahaka mzuri na watu

Apply for this position


Afisa Uhifadhi wa Bahari Daraja la II-UNGUJA

Posts: 3  |  Closing: Jun 16, 2026 Apply  |  Period: 02/06/2026 - 16/06/2026  |  Scale: ZPSF 02

Duties and Responsibilities

  • Kushajihisha na kuratibu uwekezaji wa uhifadhi wa baharini katika ngazi ya Wilaya/Mkoa;
  • Kuratibu shughuli za uanzishaji wa maeneo mapya ya hifadhi ya bahari;
  • Kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya jamii katika uhifadhi wa maeneo ya baharini;
  • Kuratibu na kushajihisha jamii katika uhifadhi wa maeneo ya bahari;
  • Kuratibu shughuli za uanzishaji wa maeneo ya hifadhi ya Bahari;
  • Kuratibu na kuendeleza maeneo ya hifadhi ya bahari;
  • Kuratibu shughuli za kufanya tafiti zinazohusiana na uendelezaji na uhifadhi wa maendeleo ya bahari;
  • Kuwajengea uelewa Wadau kuhusu uhifadhi na fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo ya bahari;
  • Kuanzisha na kuendeleza utalii endelevu wa Bahari;
  • Kusimamia doria katika maeneo ya hifadhi za bahari;
  • Kuendeleza maeneo ya urithi yalio ndani ya maeneo ya hifadhi ya Bahari;
  • Kuwaelimisha wananchi juu matumizi endelevu ya rasilimali za bahari;
  • Kufanya ukaguzi katika maeneo ya uhifadhi bahari ili kudhibiti matumizi haramu katika maeneo ya hifadhi;
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka; na
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

Qualifications

Awe Mzanzibari awe na umri usiozidi miaka 46

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Sayansi ya Bayalojia ya Bahari (Science in Marine Bialogy) au Sayansi ya Bahari (Marine Science) au Sayansi ya Mazingira ( Environmental Science) au Sayansi ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Science and Management) au Jiografia na  Mazingira (Geography and Environmental Studies) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Awe na mlahaka mzuri na watu

Apply for this position


Afisa Uchumi wa Buluu Daraja la II-UNGUJA

Posts: 1  |  Closing: Jun 16, 2026 Apply  |  Period: 02/06/2026 - 16/06/2026  |  Scale: ZPSF - 02

Duties and Responsibilities

  • Kukuza sekta ya uchumi wa Bluu ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi Zanzibar;
  • Kuandaa sera, mipango na mikakati ya kitaifa ya kukuza sekta ya uchumi wa Buluu kwa kushirikisha wadau wa sekta husika pamoja na kusimamia utekelezaji wake kikamilifu;
  • Kuzileta pamoja taasisi na asasi zinazohusika na sekta ya uchumi wa Bluu kwa lengo la kuoanisha sera, mipango na mikakati yao kwa maendeleo ya sekta za uchumi wa Buluu Zanzibar;
  • Kuainisha mahitaji ya miundo mbinu pamoja na kushajihisha taasisi na asasi za sekta ya uchumi wa Bluu kutumia miundo mbinu iliopo kwa ushirikiano ili kukuza sekta ya uchumi wa Bluu Zanzibar;
  • Kushiriki katika majukwaa ya kitaifa, kikanda na kimataifa yanayohusu maendeleo ya Uchumi wa Bluu;
  • Kupokea, kutunza na kutoa takwimu na taarifa zinazohusiana na maendeleo ya sekta ya uchumi wa Bluu Zanzibar (dashboard);
  • Kuanzisha, kukuza na kuratibu uendeshaji wa mfuko maalum kwa maendeleo ya uchumi wa Bluu Zanzibar;
  • Kuratibu tafiti na mafunzo yanazohusiana na sekta ya uchumi wa Bluu ili kuiendeleza sekta hio Zanzibar;
  • Kutoa uelewa kwa taasisi za umma, taasisi binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya shughuli zinazohusiana na sekta ya Uchumi wa Bluu Zanzibar.
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka; na
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

Qualifications

Awe Mzanzibari awe na umri usiozidi miaka 46

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani Uvuvi, Kilimo na Ufugaji wa Viumbe Maji (Fisheries and Aquaculture) au Sayansi ya Bahari (Marine Science) au Sayansi ya Bayalojia ya Bahari (Science in Marine Bialogy) au Sayansi ya Mazingira (Environmental Science) au Sayansi ya  Ufugaji wa Viumbe Maji ( Aquaculture) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Awe na mlahaka mzuri na watu

Apply for this position


Afisa TEHAMA Daraja la II-UNGUJA

Posts: 1  |  Closing: Jun 16, 2026 Apply  |  Period: 02/06/2026 - 16/06/2026  |  Scale: ZPSG - 08

Duties and Responsibilities

  • Kufanya majaribio ya sehemu timilifu za program za Kompyuta (Perform Unit Systems (Module Testing),
  • Kufanya majaribio ya mifumo ya TEHAMA (Perform Esting of System Configurations),
  • Kufanya majaribio ya program za Kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji (Conducting User Acceptance Test),
  • Kuweka usalama wa Vifaa vya TEHAMA ndani ya Wizara.
  • Kuzitunza na kuzihakiki taarifa za Taasisi kwa Matumizi ya Serikali.
  • Kuweka kumbukumbu za miundombinu ya TEHAMA.
  • Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

Qualifications

Awe Mzanzibari awe na umri usiozidi miaka 46

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Communication Technology) Teknolojia ya Habari (Information Technology) au Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)  kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Awe na mlahaka mzuri na watu

Apply for this position


Afisa Uvuvi Daraja la II-UNGUJA

Posts: 3  |  Closing: Jun 16, 2026 Apply  |  Period: 02/06/2026 - 16/06/2026  |  Scale: ZPSF - 02

Duties and Responsibilities

  • Kushiriki katika kuweka Takwimu za Uvuvi wa samaki pamoja na mazao mengine ya baharini;
  • Kuthibitisha ya kwamba zana za Uvuvi zinazotumiwa zinafuata Viwango vilivyowekwa;
  • Kuwashajihisha wananchi hasa wa vijijini katika ujenzi wa mabwawa na ufugaji wa samaki.
  • Kuthibitisha malipo ya leseni kwa vyombo vya uvuvi.
  • Kusaidia kusimamia, kukuza, kuendeleza, kudhibiti na kufuatilia shughuli za uvuvi;
  • Kusaidia kufanya tafiti za kisayansi juu ya masuala ya uvuvi;
  • Kuinua uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira ya bahari na rasilimali zake;
  • Kusaidia kuanzisha na kutekeleza sheria na kanuni za kulinda mazingira ya bahari;
  • Kuwajengea uwezo wavuvi kwa kuwapatia teknologia bora na kuwapa vifaa vya kisasa;
  • Kusaidia kuanzisha maeneo ya kukusanya samaki na mitambo ya   kuzalisha barafu kwa kuhifadhi samaki katika maeneo ya uvuvi.
  • Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yako kama utakavyopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

Qualifications

Awe Mzanzibari awe na umri usiozidi miaka 46

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Ufugaji wa Viumbe Maji na Uvuvi (Aquaculture and Fisheries)  au Sayansi ya Bahari (Marine Science) au Bayolojia ya Bahari (Marine Biology) au Sayansi ya Ufugaji wa Viumbe Maji (Aquaculture Science) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Awe na mlahaka mzuri na watu

Apply for this position