Nafasi: Dereva wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (BRT)
Idadi ya Nafasi: 200
Daraja la Mshahara: Grade 4
Uzoefu: Angalau Miaka 3
Mwisho wa Kutuma Maombi: 9 Oktoba 2026
MUHTASARI WA KAZI
Dereva wa Basi la Mwendokasi (BRT) atawajibika kuendesha basi la mwendokasi kwa usalama, umakini na weledi, kwa kuzingatia ratiba, njia na vituo vilivyopangwa.
Pia atahakikisha usalama wa abiria, kufanya ukaguzi wa basi, kuzingatia sheria za barabarani na taratibu za BRT, pamoja na kutoa huduma bora kwa abiria.
SIFA ZA MWOMBAJI
Muombaji anatakiwa kuwa na:
- Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne (IV) na Kidato cha Sita (VI).
- Leseni ya Udereva Daraja C Plain iliyohakikiwa na Jeshi la Polisi.
- Cheti cha PSV kutoka VETA au NIT.
- Cheti cha BRT kutoka NIT.
- Uzoefu wa kazi wa angalau miaka 3 katika udereva wa magari ya abiria au mabasi.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuendesha basi la mwendokasi kwa usalama, umakini na kuzingatia ratiba na vituo vilivyopangwa.
- Kuhakikisha usalama wa abiria, watumiaji wengine wa barabara na mali wakati wote wa safari.
- Kufanya ukaguzi wa basi kabla na baada ya safari ili kuhakikisha liko katika hali nzuri na salama kwa matumizi.
- Kuripoti mara moja hitilafu za kiufundi, ajali, matukio au changamoto nyingine zinazojitokeza wakati wa safari kwa msimamizi husika.
- Kuhakikisha basi linatunzwa, linakuwa safi na katika hali nzuri wakati wote wa matumizi.
- Kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, taratibu za BRT na miongozo ya kampuni.
- Kutoa huduma bora kwa abiria kwa heshima, staha na weledi.
- Kufuatilia muda wa mwisho wa uhalali wa nyaraka za dereva na kutoa taarifa kwa wakati kabla ya nyaraka hizo kuisha muda wake.
- Kuhifadhi na kuwasilisha kwa usahihi taarifa za safari, matumizi ya nishati ya gesi na taarifa nyingine muhimu za uendeshaji wa basi.
- Kutoa msaada na kufuata taratibu za usalama wakati wa dharura, ajali au matukio mengine yasiyotarajiwa.
- Kuwa makini zaidi katika maeneo yenye vivuko vya waenda kwa miguu (zebra), vituo vya BRT na maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
- Kushirikiana na wasimamizi, waendeshaji wenzake na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha huduma ya usafiri inatolewa kwa ufanisi na kwa usalama.
DARAJA LA MSHAHARA
Grade 4
Mwisho wa Kutuma Maombi: 9 Oktoba 2026
Mofat Company Limited is a Tanzanian logistics and transportation firm based in Dar es Salaam, with over 25 years of experience in providing supply chain solutions.
Services Offered
- Transportation: Road, air, and sea transport solutions tailored to business needs, with flexible options.
- Logistics & Warehousing: Streamlined supply chain operations using tech-driven tracking and optimized routing.
- Shipping: Local and international freight services with real-time monitoring.
- BRT Operations: Key player in Dar’s Bus Rapid Transit Phase II awarded a 12-year contract to operate the Gerezani to Mbagala corridor with 255 natural gas powered buses by August 2025
- Location
- Dar es salaam
- Website
- www.mofat.co.tz/