Job Role Insights

  • Date posted

    2026-09-03

  • Closing date

    2026-09-17

  • Hiring location

    Tanzania

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Certificate Degree Diploma High School Certificate O-Level Secondary Education Vocational / Technical

  • Experience

    1 - 2 Years

  • Quantity

    564 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    143387

Job Description

The total number of job posts listed here for the Ministries, Departments, Agencies and Local Government Authorities (MDAs & LGAs) is 564 posts in September 2026.

This nationwide public sector recruitment targets education, medical services, nursing, veterinary and livestock development, dental therapy, laboratory technology, forestry, environmental health, and office secretarial management.

Job Title / SpecializationPosts
Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II (Assistant Nursing Officer Grade II)128
Daktari Daraja la II (Medical Officer Grade II)115
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II)74
Mwalimu Daraja la III C - Somo la Hisabati (Mathematics Teacher Grade III C)67
Mwalimu Daraja la III C - Somo la Fizikia (Physics Teacher Grade III C)55
Mwalimu Daraja la III B - Somo la Hisabati (Mathematics Teacher Grade III B)48
Mwalimu Daraja la III B - Somo la Fizikia (Physics Teacher Grade III B)43
Afisa Mifugo Daraja la II (Livestock Officer Grade II)39
Afisa Misitu Msaidizi Daraja la II (Assistant Forest Officer Grade II)28
Mteknolojia Maabara Daraja la II (Health Laboratory Technologist Grade II)25
Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II (Assistant Environmental Health Officer Grade II)26
Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II (Dental Therapist Grade II)17
Mwalimu Daraja la III C - Somo la Fasihi ya Kiingereza (English Literature Teacher Grade III C)13
TOTAL POSTS564

MDAs & LGAs

Vacancies: 564  |  Latest closing: 17/09/2026

MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA FASIHI YA KIINGEREZA (ENGLISH LITERATURE SUBJECT)

Posts: 13  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGTS-D

Duties and Responsibilities

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

Qualifications

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fasihi ya Kiingereza

AU

Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fasihi ya Kiingereza pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu  ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


DAKTARI DARAJA LA II (MEDICAL OFFICER GRADE II)

Posts: 115  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGHS E

Duties and Responsibilities

  • Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
  • Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  • Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
  • Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
  • Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
  • Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
  • Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
  • Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
  • Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
  • Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
  • Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality   improvement).

Qualifications

Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

Apply for this position


AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT NURSING OFFICER GRADE II)

Posts: 128  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGHS-B

Duties and Responsibilities

  • Kutoa huduma za uuguzi.
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Qualifications

Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

Apply for this position


AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK OFFICER GRADE II)

Posts: 39  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGS.D

Duties and Responsibilities

  • Kubuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani;
  • Kuratibu uzalishaji wa mifugokatikamashamba madogo na makubwa ya mifugo;
  • Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani;
  • Kuratibuna kuendesha mafunzo ya ufugajibora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalam wa mifugo na wafugaji;
  • Kufanyamapitio na marekebisho ya miundombinu ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani;
  • Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani;
  • Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) k.m. mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi;
  • Kuendesha mafunzokwa mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo;
  • Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali;
  • .Kufanya tathmini juu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na ufugaji katika wilaya;
  • .Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho;
  • Kufuatilia,kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo;
  • Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo;
  • .Kufanya kazi nyingine zinazohusianana fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

Qualifications

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Sayansi ya Kilimo waliobobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Apply for this position


TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (DENTAL THERAPIST GRADE II)

Posts: 17  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGHS B

Duties and Responsibilities

  • Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi.
  • Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida.
  • Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo.
  • Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi.
  • Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa Afya ya Jamii.
  • Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
  • Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

Qualifications

Kuajiriwa wenye Stashahada ya Tabibu wa Meno (Diploma in Clinical Dentistry) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, pia awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari.

Apply for this position


MTEKNOLOJIA MAABARA DARAJA II ( HEALTH LABORATORY TECHNOLOGIST GRADE II)

Posts: 25  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGHS B

Duties and Responsibilities

  • Kupima sampuli zinazoletwa maabara.
  • Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara za ngazi za juu.
  • Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi, vifaa, kemikali na hifadhi ya kemikali.
  • Kuweka kumbukumbu za maabara ambazo zimepatikana wakati wa uchunguzi.
  • Kufundisha watumishi walio chini yake.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

Qualifications

Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara za afya kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, ambao wamesajiliwa na Baraza la Waatalam wa Maabara.

Apply for this position


MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA FIZIKIA (PHYSICS SUBJECT)

Posts: 55  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGTS- D

Duties and Responsibilities

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

Qualifications

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fizikia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fizikia  pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu  ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA HISABATI (MATHEMATICS SUBJECT)

Posts: 67  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGTS- D

Duties and Responsibilities

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

Qualifications

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Hisabati

AU

Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Hisabati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu  ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


MWALIMU DARAJA LA III B - SOMO LA FIZIKIA (PHYSICS SUBJECT)

Posts: 43  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGRS C

Duties and Responsibilities

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za  Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa  ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

Qualifications

Kuajiriwa wahitimu wenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Fizikia kutoka  Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


MWALIMU DARAJA LA III B - SOMO LA HISABATI (MATHEMATICS SUBJECT)

Posts: 48  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGTS-C

Duties and Responsibilities

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za  Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa  ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

Qualifications

Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


AFISA MISITU MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT FOREST OFFICER GRADE II)

Posts: 28  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGS C

Duties and Responsibilities

  • i. Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
  • ii. Kukusanya takwimu za misitu.
  • iii. Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
  • iv. Kukusanya maduhuli.
  • v. Kupima mazao ya misitu.
  • vi. Kufanya doria.
  • vii. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake;

Qualifications

Kuajiriwa wenye Stashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo; Forestry, Agroforestry, Forest Resources Assessment and Management, Forest Biology, Forest Economics, Forest Engineering au fani nyingine inayoendana na hiyo kutoka katika Taasisi au Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

Apply for this position


AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT ENVIRONMENTAL HEALTH OFFICER GRADE II)

Posts: 26  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGHS B

Duties and Responsibilities

  • i. Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa;
  • ii. Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa;
  • iii. Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa ya kuambukiza;
  • iv. Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na kuziwasilisha katika mamlaka husika;
  • v. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili;Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii;
  • vi. Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha usalama na afya ya jamii;
  • vii. Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo;
  • viii. Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira;
  • ix. Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi ya Kata; na
  • x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Qualifications

Kuajiriwa wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.

Apply for this position


MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY GRADE II)

Posts: 74  |  Closing: 17/09/2026  |  Period: 03/09/2026 - 17/09/2026  |  Scale: TGS C

Duties and Responsibilities

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika;.
  • Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; naix.
  • Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Qualifications

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies). Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100(100.w.p.m) kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Apply for this position

Interested in this job?

13 days left to apply

Apply now

Your job search, in your pocket

Get the ZoomTanzania Jobs app - apply on the go, get instant job alerts, and chat with our AI assistant anytime, anywhere.

How to Apply

Apply now