Afisa Mipango Daraja la II Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Job Role Insights
-
Date posted
2026-06-12
-
Closing date
2026-06-25
-
Hiring location
Zanzibar
-
Career level
Middle
-
Qualification
Certificate Degree Diploma
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
1 person
-
Gender
both
-
Job ID
135468
Job Description
POST: Afisa Mipango Daraja la II – PEMBA (Nafasi 1)
MWAJIRI: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
MUDA WA MAOMBI: Kuanzia tarehe 11/06/2026 hadi 25/06/2026
MAJUKUMU NA WAJIBU
- Kupitia na kuchambua mpango wa miaka mitano wa Rasilimali Watu ili kuhakikisha unatekelezeka kwa ufanisi.
- Kupitia na kutathmini uwezo wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kubaini mahitaji halisi ya watumishi.
- Kuainisha mahitaji ya ziada ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma kulingana na mahitaji ya taasisi husika.
- Kutayarisha Ikama na kufanya mapitio yake kwa kuzingatia mabadiliko ya kiutendaji.
- Kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi ikiwemo taarifa za robo mwaka, nusu mwaka na mwaka.
- Kushiriki katika ukusanyaji, uchambuzi na uhifadhi wa takwimu zinazohusu mipango na rasilimali watu.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya mipango kwa mujibu wa sera, sheria na miongozo iliyopo.
- Kushiriki katika ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya kazi ndani ya taasisi.
- Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46.
- Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe na uwezo mzuri wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto zinazohusiana na mipango.
- Awe na uwezo wa kuandaa na kuwasilisha taarifa mbalimbali za kiutendaji.
- Awe na ujuzi wa matumizi ya kompyuta, hususan programu za ofisi.
- Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano na kufanya kazi kwa ushirikiano na wengine.
- Awe mwaminifu, mwenye nidhamu na anayezingatia maadili ya Utumishi wa Umma.
MSHAHARA
- ZPSF 02.
Interested in this job?
This job has expired
Your job search, in your pocket
Get the ZoomTanzania Jobs app - apply on the go, get instant job alerts, and chat with our AI assistant anytime, anywhere.
