Nafasi za Kazi 14 Mbarali District Council
Job Role Insights
-
Date posted
2025-11-10
-
Closing date
2025-11-20
-
Hiring location
Mbeya
-
Career level
Middle
-
Qualification
Bachelor Degree Diploma
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
124940
Job Description
Mbarali District Council is the local government authority (LGA) responsible for administering the Mbarali District in Tanzania's Mbeya Region, with its headquarters in Rujewa. It operates as a council to promote social welfare and economic development within its jurisdiction, focusing on areas like rice farming and environmental preservation.
The total number of job posts listed here for the Mbarali District Council (Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali) is 14 posts in November 2025.
| Job Title | Posts |
| 1.0 Records Assistant Grade II | 4 |
| 2.0 Office Secretary Grade II | 5 |
| 3.0 Driver Grade II | 5 |
| TOTAL POSTS | 14 |
Kumb. Na. MDC/S.20/VOL.VII/5/13
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Mbarali anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na nne (14) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II - NAFASI 04 (Records Assistant Grade II - 4 Positions)
- MAJUKUMU YA KAZI (Job Responsibilities)
- Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Regista (Incomming Correspondence Register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu / Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
SIFA ZA MWOMBAJI (Applicant Qualifications)
- Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (IV) na kupata cheti cha mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
- Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma NTA level 6 katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, pia awe na ujuzi wa kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA (Salary Scale)
TGS C
2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 05 (Office Secretary Grade II - 5 Positions)
MAJUKUMU YA KAZI (Job Responsibilities)
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/kitengo/sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI (Applicant Qualifications)
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) katika ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya uhazili.
- Aidha wawe wamefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA (Salary Scale)
TGS C
DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 05 (Driver Grade II - 5 Positions)
MAJUKUMU YA KAZI (Job Responsibilities)
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari "logbook" kwa safari zote.
- Kufanya usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI (Applicant Qualifications)
- Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni Daraja 'E' au 'C 'ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA (Salary Scale)
TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI (General Conditions for Applicants)
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates - Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI - Computer Certificate, - Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
- Waombaji watakaowasilisha "Testmonial", "Provisional Results", "Statement of results", hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji wa kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja 'E' au 'C' wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19 Novemba, 2025.
- MUHIMU: UTARATIBU WA MAOMBI (Important: Application Procedure)
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI,
S.L.P 237, RUJEWA
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/
- (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal') .
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na; MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI
Interested in this job?
10 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
