Nafasi za Kazi 4 Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale November 2025
Job Role Insights
-
Date posted
2025-11-06
-
Closing date
2025-11-18
-
Hiring location
Geita
-
Career level
Middle
-
Qualification
Bachelor Degree Certificate Degree Diploma
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
4 person
-
Gender
both
-
Job ID
124706
Job Description
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA GEITA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'HWALE FANG’HWALE DISTRICT COUNCIL NYANG’HWALE
Kumb. Na. AC.12/214/Α/23 05/11/2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Nyang'hwale anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi nne (04) za kazi katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:
The Executive Director of the Nyang'hwale District Council is inviting applications from qualified Tanzanian citizens for a total of four (04) job vacancies.
The positions open for application are:
- Office Management Secretary Grade II (Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II): 2 positions
- Records Management Assistant Grade II (Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II): 2 positions
Applications must be submitted through the electronic recruitment portal by the deadline of November 18, 2025
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY II) - NAFASI 02
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali - TGS C.
2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II) - NAFASI 02
1.2 MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register).
- Kusambaza, majalada kwa watendaji (action officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
- Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
- Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
- Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
1.2.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada (Diploma) au Cheti cha NTA level 6 katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.
1.2.2 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali - TGS C.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate.
- Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
- "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Novemba, 2025.
- Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal').
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFANYIWI KAZI.
MUHIMU: KUMBUKA kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
- Mkurugenzi Mtendaji
- Halmashauri ya Wilaya,
- S.L.P 352,
- NYANG'HWALE
Limetolewa na; Husna Toni MKURUGENZI MTENDAJI (W) NYANG'HWALE
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyang'hwale, S. L. P. 352, Mkoa wa Geita, Barua pepe:[email protected] Tovuti: www.nyanghwale.go.tz
Interested in this job?
12 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
