Jobs at RUWASA Handeni (10 Vacancies)

Job Role Insights

  • Date posted

    2025-03-06

  • Closing date

    2025-03-06

  • Hiring location

    Tanga

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Degree Diploma

  • Experience

    1 - 2 Years 3 Years

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

Job Description

Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Handeni kwa niaba ya Vyombo vya watoaji huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs), inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

  • Wasimamizi wa CBWSO (2).
  • Mafundi wasaidizi wa skimu za maji (7).
  • Mhasibu (1)

Watumishi hao watafanya kazi kwenye vyombo (5) vya utoaji huduma ya  maji ngazi    ya   jamii ambavyo ni:-

  • MMWaSSO
  • MSOMERA
  • KWAMSISI - KWASUNGA
  • KWAMGWE
  • KANG’ATA

    SIFA ZA MSIMAMIZI MKUU WA CBWSO.

    • Awe na elimu kuanzia kidato cha nne (4) na kuendelea
    • Awe na astashahada au stashahada ya ufundi katika fani ya Maji au fani inayohusiana kutoka chuo kinacho tambulika na Serikali.
    • Awe na umri kuanzia miaka 18- 45
    • Awe mwaminifu ambaye hajawahi kushtakiwa kwa makosa ya jinai. V. Awe na uzoefu kwenye kazi za Sekta ya maji.
    • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

    MAJUKUMU YA MSIMAMIZI MKUU

    • Atakuwa ndie msimamizi mkuu wa chombo cha utoaji huduma ya maji ngazi ya      jamii, pia atakuwa Katibu wa Kamati ya Maji na Mtendaji mkuu wa shughuli za chombo.
    • Atawajibika kwa Kamati ya Chombo cha utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) kwa   shughuli za kila siku.
    • Atawajibika na kusimamia shughuli zote za matengenezo, ufundi na   usimamizi wa vifaa vya ufundi wa shughuli hizo.
    • Kusimamia Ankara za maji na kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wote wanao hudumiwa na chombo.
    • Atawajibika kutoa taarifa zote za kiutendaji kwa Meneja wa RUWASA(W) kwa kadiri atakavyo elekezwa.
    • Kuandaa taarifa zote za mapato na matumizi, pamoja na mihutasari ya vikao vya  mwezi,  robo na  kuwasilisha kwa Meneja  RUWASA (W).
    • Kuhamasisha wananchi kulipia bili za maji na kutatua migogoro kati ya chombo na   wananchi.
    • Kufanya manunuzi ya mahitaji ya mradi wa chombo kwa kufuata miongozo ya manunuzi
    • Awe tayari kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa.

    MSHAHARA

    Kazi hii ni ya mkataba na mshahara utalipwa kutokana na makusanyo ya mauzo ya maji kwa mradi husika na utaidhinishwa na Kamati ya Maji ya chombo husika (CBWSO).

    FUNDI BOMBA MSAIDIZI

    • Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
    • Awe na cheti cha Elimu ya ufundi bomba (VETA) kutoka katika chuo chochote kinacho tambuliwa na Serikali
    • Awe na umri usiopungua miaka 18-45
    • Awe na uzoefu wa ufundi usio pungua mwaka mmoja.

     MAJUKUMU YA FUNDI MSAIDIZI

    • Kufanya kazi kama zitakavyoelekezwa fundi mkuu.
    • Kufunga bomba za aina mbali mbali za mradi wa maji na usafi wa mazingira.
    • Kufanya usafi wa miundo mbinu ya maji (Vyanzo vya maji na Matangi)
    • Kufanya matengenezo ya bomba,kuziba mivujo,kusoma dira za maji na kufuata ratiba za dharula zinapojitokeza
    • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Meneja.

    MSHAHARA

    Kazi hii ni ya mkataba na mshahara utalipwa kutokana na makusanyo ya mauzo ya maji kwa mradi husika na utaidhinishwa na Kamati ya Maji ya chombo husika (CBWSO). (CBWSO).

    MHASIBU 

    • Awe na elimu kuanzia kidato cha nne (4) na kuendelea.
    • Awe na Astashahada au Stashada katika fani ya uhasibu kutoka chuo chochote kinacho tambulika na Serikali.
    • Awe na umri kuanzia miaka18-45
    • Awe na uwezo wa kufanya ulinganifu wa taarifa za Kifedha V.    Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
    • Awe mwadilifu na asie wahi kushitakiwa kwa kosa lolote la wizi au jinai

    MAJUKUMU YA MHASIBU 

    • Kupeleka fedha zote Benki za makusanyo ya bili za maji na mapato mengine kabla ya matumizi.
    • Kushauriana na msimamizi wa chombo katika masuala yote yanayohusu fedha.
    • Kufanya malipo baada ya kuidhinishwa na chombo. 
    • Kutunza kumbukumbu zote na nyaraka zote zinazo husu fedha kwenye chombo.
    • Kuandaa taarifa zote za fedha mapato na matumizi na kuziwasilisha kwa msimamizi.
    • Kufanya majukumu mengine atakayo pangiwa na Msimamizi wa chombo.

    MSHAHARA

    Kazi hii ni ya mkataba na mshahara utalipwa kutokana na makusanyo ya mauzo ya maji kwa mradi husika na utaidhinishwa na Kamati ya Maji ya chombo husika (CBWSO).

    (CBWSO).

    NB: Wanawake watapatiwa kipaumbele

    MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

    • Maombi yaambatane na vivuli vya vyeti vya masomo na mafuzo pamoja na picha tatu(Pasport Size) za hivi karibuni.
    • Muombaji awe tayari kufanya kazi CBWSO yoyote atakayo pangiwa.
    • Waombaji waambatanishe wasifu wao binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu za muombaji, barua pepe, pamoja na wadhamini watatu.
    • Muombaji ambaye tayari ni mwajiriwa katika utumishi wa Umma asiombe nafasi hizi.
    • Uwasilishaji wa taarifa za kughushi ikiwemo vyeti feki waombaji watachukuliwa hatua kali za kisheria.
    • Maombi yaambatane na nakala ya cheti cha kuzaliwa.
    • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/03/2025 saa 9:30 Alasiri.
    • Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwa kutumia anuani hii:- 

    Meneja wa RUWASA(W),

    S.L.P 47, Handeni.

    Interested in this job?

    0 days left to apply

    Apply now

    Share this opportunity

    Help others find their dream job

    How to Apply

    MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI Maombi yaambatane na vivuli vya vyeti vya masomo na mafuzo pamoja na picha tatu(Pasport Size) za hivi karibuni. Muombaji awe tayari kufanya kazi CBWSO yoyote atakayo pangiwa. Waombaji waambatanishe wasifu wao binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu za muombaji, barua pepe, pamoja na wadhamini watatu. Muombaji ambaye tayari ni mwajiriwa katika utumishi wa Umma asiombe nafasi hizi. Uwasilishaji wa taarifa za kughushi ikiwemo vyeti feki waombaji watachukuliwa hatua kali za kisheria. Maombi yaambatane na nakala ya cheti cha kuzaliwa. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/03/2025 saa 9:30 Alasiri. Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwa kutumia anuani hii:-  Meneja wa RUWASA(W), S.L.P 47, Handeni.

    Apply now
    Send message
    Cancel