Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilindi 22-06-2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 23/06/2026 hadi 24/06/2026, na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (mask).
  • Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.

Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:

  • Kitambulisho cha Mkazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Kazi
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Hati ya Kusafiria
  • Leseni ya Udereva
  • Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji anachotoka
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia:
  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Cheti cha Kidato cha IV
  • Cheti cha Kidato cha VI
  • Astashahada
  • Stashahada
  • Stashahada ya Juu
  • Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za nafasi husika
  • Wasailiwa watakaowasilisha:
  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • Form IV Results Slip
  • Form VI Results Slip

Havitakubaliwa na hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

  • Kwa kada zinazohitaji usajili wa Bodi za Kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuja na:
  • Vyeti vyao halisi vya usajili
  • Leseni za kufanyia kazi
  • Kila msailiwa atajigharamia:
  • Chakula
  • Usafiri
  • Malazi

Aidha, kila msailiwa anapaswa kuhudhuria usaili akiwa na mavazi nadhifu na yenye staha kulingana na waraka wa mavazi.

  • Wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama:
  • TCU
  • NACTVET
  • NECTA

Wasailiwa wa kada zinazohitaji GPA waliosoma nje ya Tanzania wawasilishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.

  • Wasailiwa ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili.

Aidha, wasailiwa watakaofanya usaili wa mchujo kwa njia ya mtandao wanapaswa kukumbuka:

  • Barua pepe (email address) zao
  • Nywila (password) zao

wanazotumia katika mfumo wa Ajira Portal.

  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
  • Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku:
  • Kutoa rushwa
  • Kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi.

Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya:

  • Haki
  • Usawa
  • Uwazi

kwa kuzingatia sifa stahiki zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara inayohusika.

FIND NAMES HERE