Nafasi za Kazi 43 Wizara ya Mifugo na Uvuvi (MLF)

Job Role Insights

  • Date posted

    2025-12-11

  • Closing date

    2025-12-23

  • Hiring location

    Tanzania

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Degree Diploma Secondary Education Vocational / Technical

  • Experience

    2 Years

  • Quantity

    10 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    126152

Job Description

The Ministry of Livestock and Fisheries (MLF) is a key government body in Tanzania responsible for developing, managing, and regulating the country's livestock and fisheries sectors, aiming for sustainability, commercialization, and improved livelihoods, food security, and national income through policy guidance, capacity building, and private sector support.

The total number of job posts listed here for the Ministry of Livestock and Fisheries (Wizara ya Mifugo na Uvuvi) is 43 posts in December 2025.

Job TitlePosts
1.0 Fish Technologist II (MTEKNOLOJIA WA SAMAKI DARAJA LA II)3
2.0 Veterinary Officer II (DAKTARI WA MIFUGO II)19
3.0 Livestock Research Officer II (AFISA UTAFITI MIFUGO DARAJA LA Il)1
4.0 Livestock Field Assistant (MSAIDIZI WA MIFUGO)20
TOTAL POSTS43

1.0 MTEKNOLOJIA WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGIST II) - 3 Posts

Majukumu ya Kazi:

  • Kutoa ushauri juu ya utayarishaji, uchakataji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki na mazao ya uvuvi;
  • Kukagua na kusimamia ubora wa mazao ya uvuvi na mwani kulingana na viwango vya kitaifa ana kimataifa;
  • Kusimamia na kushauri kuhusu Kanuni za udhibiti ubora wa mazao ya uvuvi na mwani;
  • Kudhibiti ubora wa samaki katika mialo, masoko, viwanda na maghala;
  • Kudhibiti usafi katika maeneo ya kupokelea samaki na mwani;
  • Kukagua viwanda vinavyochakata, maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi na vyombo vya usafirishaji wa mazao ya uvuvi kulingana na "HACCP" (Hazard Analysis Critical Control Point);
  • Kuhakiki nyaraka mbalimbali za uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya uvuvi na mwani; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa Kitengo zinazohusiana na fani yake.

Sifa za Mwombaji:

Kuajiriwa wenye mojawapo wa Shahada za fani za Fish Technology, Marine Biology and Applied Microbiology, Fisheries Sciences and Microbiology kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Sayansi ya Chakula (Food Technology and Microbiology) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara:

TGS D

2.0 DAKTARI WA MIFUGO II (VETERINARY OFFICER II) - 19 Posts

Majukumu ya Kazi:

  • Kutoa huduma za afya ya mifugo;
  • Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo lake la kazi kwa mujibu wa sheria;
  • Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake;
  • Kusimamia haki za wanyama;
  • Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake;
  • Kusimamia na kuratibu uzingatiaji wa Kanuni na Sheria za Magonjwa, ukaguzi wa mifugo na mazao yake na pembejeo za mifugo;
  • Kuratibu na kusimamia shughuli za usafi wa machinjio na ukaguzi wa nyama katika eneo lake la kazi;
  • Kuandaa taarifa ya afya ya mifugo katika eneo lake la kazi; na
  • Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Sifa za Mwombaji:

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Tiba ya Wanyama (Veterinary Medicine) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali ambao wamesajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania.

Ngazi ya Mshahara:

TGSA

3.0 AFISA UTAFITI MIFUGO DARAJA LA Il (LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) - 1 Post

Majukumu ya Kazi:

  • Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi;
  • Kuandika na Kuweka kumbukumbu za utafiti;
  • Kusaidia kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora;
  • Kuandaa mapendekezo ya utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayemsimamia; na
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

Sifa za Mwombaji:

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani ya Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara:

TGRS A

4.0 MSAIDIZI WA MIFUGO (LIVESTOCK FIELD ASSISTANT) - 20 Posts

Majukumu ya Kazi:

  • Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji wa mifugo na mazao yake;
  • Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa, tiba na chakula;
  • Kusimamiza utendaji kazi wa Wahudumu Mifugo;
  • Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za mifugo;
  • Kukagua ubora wa mazao ya mifugo;
  • Kusimamia ustawi wa wanyama; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.

Sifa za Mwombaji:

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI ambao wamepata mafunzo ya mifugo na kutunukiwa Astashahada ya Afya ya Mifugo na Uzalishaji (NTA Level 5) kutoka Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency - LITA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara:

TGS B

Interested in this job?

12 days left to apply

Apply now

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

Apply now
Send message
Cancel