Nafasi ya Kazi Mtaalamu wa Mifumo ya Chakula Katika Maendeleo ya Sekta ya Mpunga

Job Role Insights

  • Date posted

    2025-11-07

  • Closing date

    2025-11-20

  • Hiring location

    Dodoma

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Certificate Degree Diploma Master’s Degree O-Level

  • Experience

    7 Years

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    124732

Job Description

This specialist position is part of the 5-year GEF FOLUR Impact Program project, "Food Systems, Land Use and Restoration in Tanzania’s Forest Landscapes," implemented by the Ministry of Natural Resources and Tourism with support from the World Wildlife Fund (WWF).

The primary goal of the role is to lead, guide, and support the implementation of Component 2 of the project, which focuses on developing sustainable and socially inclusive value/supply chains for the rice production sector in two key landscapes: the Kilombero Valley and North Unguja (Zanzibar). The specialist will work to create supporting policy frameworks, financial mechanisms, and market incentives to drive these sustainable value chains. The successful candidate will report to the Project Coordinator and is required to have at least 7 years of technical experience and a post-graduate degree in a relevant field. The application deadline is November 20, 2025.

UTANGULIZI WA MRADI

Mradi wa 'Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Marejesho ya Maeneo ya Misitu Nchini Tanzania' (The Project ‘Food Systems Land Use and Restoration in Tanzania’s Forest Landscapes’) ni Mradi mtoto chini ya Mpango wa Athari wa GEF wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Marejesho (FOLUR Impact Program). Mradi huu wa miaka 5 unatekelezwa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, kama Shirika Kiongozi Mtekelezaji, kwa ushirikiano na Shirika la Hifadhi ya Wanyamapori Duniani (WWF) kama Shirika Tekelezi la GEF.

Tatizo kuu la kimazingira ambalo linapaswa kushughulikiwa na mradi huu ni uharibifu wa ardhi yenye misitu na maeneo oevu yenye utajiri nchini Tanzania na upotevu unaohusiana wa afya ya misitu na bioanuwai, chini ya shinikizo la maendeleo ya kilimo, kwa kuzingatia uzalishaji wa mpunga, ambao una athari mbaya katika utoaji wa huduma za ikolojia na fursa zinazohusiana za maisha na kiuchumi. Nchini Tanzania, uzalishaji wa mpunga umeongezeka zaidi ya mara tatu kati ya mwaka 2004 na 2015, na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa pili kwa ukubwa wa mpunga Kusini-Mashariki mwa Afrika. Sekta ya mpunga kwa sasa ni sehemu muhimu inayopewa kipaumbele na mipango mbalimbali inayoungwa mkono na Serikali na wafadhili inayoelekezwa katika kuongeza uzalishaji na upanuzi wa mashamba, ikiwa na nia inayoongezeka ya kuuza nje ya nchi ili kusambaza nchi jirani za Afrika. Changamoto kuu ni kwamba uzalishaji ni mdogo, ambapo mavuno ya sasa ni kati ya chini kabisa duniani (kati ya tani 1.5 na 2 kwa hekta), minyororo ya usambazaji isiyofaa, utunzaji duni wa mazao baada ya kuvuna na mtandao mbaya wa usafirishaji, jambo ambalo linaongeza changamoto zaidi.

Mradi unalenga hasa katika maeneo makuu mawili nchini Tanzania, yote muhimu kwa kilimo cha mpunga: Bonde la Kilombero Tanzania Bara; na eneo la Kaskazini Unguja (Zanzibar). Mradi huu unawakilisha mfumo jumuishi unaounganisha masuala ya mifumo endelevu ya chakula na minyororo ya usambazaji isiyosababisha ukataji miti, na mipango pana ya ngazi ya mazingira, usimamizi na urejeshaji kwa ajili ya kuhifadhi huduma za ikolojia katika maeneo haya mawili, ambayo hutafsiriwa katika nguzo tatu kuu za kazi:

  • Kuendeleza mbinu ya Usimamizi Jumuishi wa Mazingira (Integrated Landscape Management) kwa maeneo lengwa, kupitia mchakato wa wadau mbalimbali, ili kutoa mfumo wa usimamizi wa mazingira unaotoa nafasi kwa uzalishaji wa mpunga na matumizi mengine, huku ukihakikisha nafasi ya kuhifadhi na kurejesha mifumo muhimu ya ikolojia.
  • Kuendeleza minyororo ya thamani/usambazaji endelevu na jumuishi kijamii kwa sekta ya uzalishaji wa mpunga, ikiwa ni pamoja na kuendeleza mifumo ya utawala/sera, mifumo ya kifedha na masoko, na vivutio vinavyosaidia kuendesha minyororo ya thamani endelevu.
  • Kuendeleza na kutekeleza shughuli madhubuti za urejeshaji na usimamizi wa mazingira katika maeneo lengwa, ikiwa ni pamoja na kuunda mazingira wezeshi kwa ajili ya upanuzi. Lengo kuu hapa litakuwa kwenye maeneo yaliyoharibiwa na au yanayotoa huduma muhimu za kimazingira kwa sekta ya mpunga.

MASHARTI YA KAZI

Nafasi: Mtaalamu wa Mifumo Endelevu ya Chakula Katika Maendeleo ya Sekta ya Mpunga Anamripoti: Mratibu wa Mradi, Mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Marejesho Tanzania (Wizara ya Maliasili na Utalii, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) Mahali: Dodoma, Tanzania Muda: Mwaka 1, inaweza kuongezwa hadi miaka 4


KAZI KUU

Mtaalamu wa Mifumo Endelevu ya Chakula Katika Maendeleo ya Sekta ya Mpunga atatoa uongozi, mwongozo na msaada katika utekelezaji wa Kipengele cha 2 cha mradi: Kuendeleza minyororo ya thamani/usambazaji endelevu na jumuishi kijamii kwa sekta ya uzalishaji wa mpunga, ikiwa ni pamoja na kuendeleza mifumo ya utawala/sera inayounga mkono, mifumo ya kifedha na masoko, na vivutio ambavyo vitaendesha minyororo ya thamani endelevu. Hasa, atasimamia utekelezaji wa mradi kupitia Vitengo viwili vya Uratibu wa Mazingira (LCUs) huko Kilombero na Unguja, pamoja na kutoa msaada wa kiufundi unaolengwa kwa ajili ya kubuni na kutekeleza shughuli za mradi.


MAJUKUMU MAKUU

  • Kuongoza na kushauri kitaalam kuhusu utekelezaji wa Kipengele cha 2 cha mradi, hasa kuhusu:
    • Uendelezaji wa waraka wa sera juu ya umiliki bora wa ardhi na mifumo ya utawala wa maji.
    • Uandaaji wa mpango endelevu wa maendeleo ya mnyororo wa thamani kwa sekta ya uzalishaji wa mpunga.
    • Uandaaji wa miongozo, viwango, na vifurushi vya mafunzo kwa wadau wa sekta ya umma na binafsi katika minyororo ya thamani katika sekta ya mpunga.
    • Kufanya uchambuzi wa fursa kwa ajili ya uwekezaji wa sekta binafsi katika minyororo ya thamani ya uzalishaji endelevu wa mpunga.
    • Kujadiliana na kuanzisha makubaliano na jukwaa la ushirikiano kwa ajili ya ushirikishwaji kati ya wadau wa sekta ya umma, binafsi na asasi za kiraia juu ya maendeleo endelevu ya mnyororo wa thamani wa mpunga.
  • Kushauri washirika wa mradi na vitengo vya uratibu wa mazingira kuhusu usanifu wa kiufundi na utekelezaji wa shughuli za mradi chini ya Kipengele cha 2 cha mradi.
  • Kushirikiana na Kitengo cha Usimamizi wa Mradi (PMU) katika kuandaa marejeleo ya kazi (TORs) yanayohusiana na kuajiri washauri ili kuhakikisha matokeo ya kiufundi na mahitaji ya uzoefu yanajumuishwa, na katika uandaaji wa mikataba midogo kwa washirika wa mradi.
  • Kupitia ripoti na bidhaa nyingine kutoka kwa washauri, wafanyakazi, na wapokea ruzuku ndogo, na kuhakikisha ubora.
  • Kwa kushirikiana na Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (M&E), kufanya safari za mara kwa mara za uwanjani ili kufuatilia utekelezaji wa mradi na kutoa ushauri wa kiufundi na msaada kwa timu za mazingira na washirika wa mradi.
  • Kutoa mchango katika Ripoti za Maendeleo ya Mradi za nusu mwaka na za mwaka.
  • Kwa kushirikiana na Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (M&E), kuandaa bidhaa muhimu za uhamasishaji na maarifa juu ya maendeleo endelevu ya sekta ya mpunga kwa ajili ya upanuzi na uigaji.
  • Kusimamia na kuangalia ushirikishwaji wa wadau katika kipindi chote cha mradi, hasa kuhusiana na vikundi vya wakulima.
  • Kuhakikisha utekelezaji unaendana na viwango na sera za GEF na WWF.
  • Kuiwakilisha mradi, inapohitajika, katika mikutano na warsha mbalimbali.

SIFA NA MAHITAJI

  • Angalau miaka 7 ya uzoefu wa kiufundi wa kufanya kazi katika taaluma inayohusiana na Mifumo Endelevu ya Chakula hasa katika maendeleo ya sekta ya mpunga.
  • Shahada ya Uzamili (Post-graduate degree) katika taaluma inayohusiana na Mifumo Endelevu ya Chakula.
  • Uzoefu katika kusimamia miradi tata, yenye wadau mbalimbali.
  • Uwezo wa kuwasiliana na wadau wakuu wa biashara, serikali, na NGOs.
  • Ujuzi wa usimamizi unaoweza kubadilika (Adaptive management skills).
  • Uzoefu na Miradi ya GEF na ujuzi wa GEF ni faida ya ziada.

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 50.
  2. Waombaji lazima waambatishe Wasifu Binafsi wa kisasa (CV) wenye mawasiliano ya kuaminika: anwani ya posta/post code, barua pepe, na namba za simu.
  3. Waombaji wanapaswa kuomba kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa katika tangazo hili.
  4. Waombaji lazima waambatishe nakala zao za vyeti vilivyothibitishwa (certified copies) vifuatavyo:
    • Shahada ya Uzamili/Shahada/Stashahada ya Juu/Stashahada/Vyeti.
    • Hati za matokeo (transcripts) za Shahada ya Uzamili/Shahada/Stashahada ya Juu/Stashahada.
    • Vyeti vya Mitihani ya Taifa vya Kidato cha IV na Kidato cha VI.
    • Vyeti vya Usajili wa Kitaaluma na Mafunzo kutoka Bodi za Usajili au Udhibiti husika (pale inapohitajika).
    • Cheti cha Kuzaliwa.
  5. Kuambatisha nakala za vyeti vifuatavyo hakikubaliwi kabisa:
    • Hati za matokeo (results slips) za Kidato cha IV na Kidato cha VI.
    • Testimonials na hati zote za matokeo za muda (Partial transcripts).
  6. Mwombaji aliyeajiriwa katika Utumishi wa Umma anapaswa kupitisha barua yake ya maombi kwa mwajiri wake husika.
  7. Mwombaji ambaye amestaafu kutoka Utumishi wa Umma kwa sababu yoyote ile hapaswi kuomba.
  8. Mwombaji anapaswa kuonyesha wadhamini watatu (referees) wanaoaminika pamoja na mawasiliano yao.
  9. Vyeti kutoka taasisi za nje ya nchi kwa ajili ya elimu ya kawaida au ya juu vinapaswa kuhakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA).
  10. Vyeti vya kitaaluma kutoka Vyuo Vikuu vya nje na taasisi zingine za mafunzo vinapaswa kuhakikiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
  11. Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na Ielekezwe kwa:
    • Katibu Mkuu,
    • Wizara ya Maliasili na Utalii,
    • Mji wa Serikali-Mtumba,
    • Mtaa wa Ardhi
    • S.L.P. 1351,
    • DODOMA.
  12. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20 Novemba, 2025.
  13. Waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili pekee ndio watafahamishwa tarehe ya usaili.
  14. Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi na taarifa nyinginezo utapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria.

Interested in this job?

13 days left to apply

Apply now

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka hamsini. Maombi yanapaswa kuambatana na Wasifu Binafsi wa kisasa CV wenye mawasiliano ya uhakika pamoja na nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa ikiwemo Shahada ya Uzamili au Shahada, hati za matokeo za shahada, Vyeti vya Mitihani ya Taifa vya Kidato cha IV na VI, Vyeti vya Usajili wa Kitaaluma, na Cheti cha Kuzaliwa. Tafadhali kumbuka kuwa Hati za matokeo za Kidato cha IV na VI, Testimonials, na hati za matokeo za muda hazitakubaliwa. Mwombaji aliyeajiriwa serikalini anapaswa kupitisha barua yake kupitia kwa mwajiri wake, na waombaji walio staafu hawaruhusiwi kuomba. Maombi yote yaliyosainiwa yanapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na Ielekezwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, S.L.P. 1351, DODOMA. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20 Novemba, 2025.

Apply now
Send message
Cancel