Nafasi ya Kazi ya Udereva St. Jude School February 2026
Job Role Insights
-
Date posted
2026-02-16
-
Closing date
2026-02-19
-
Hiring location
Arusha
-
Career level
Middle
-
Qualification
Certificate Degree Diploma High School Certificate Secondary Education Vocational / Technical
-
Experience
2 Years
-
Quantity
1 person
-
Gender
both
-
Job ID
128139
Job Description
Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude's inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora. Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi Moja (1) ya kazi ya Udereva kwa watanzania wenye sifa stahiki.
Kazi na Majukumu
- Kuendesha magari ya shule kwa uangalifu na umakini
- Kuwa makini na kukagua mara kwa mara gari ulilokabidihiwa kuhakikisha lipo salama kabla ya na wakati wa kuliendesha
- Kutunza taarifa za gari/vipuri/mafuta na mabadiliko yoyote ikiwemo kujaza "log book" kwa usahihi na kwa kila tukio na safari za gari
- Kuripoti kwa wakati muda wa gari kukarabatiwa na/au kwenda "service"
- Kufuata taratibu sheria kanuni na miongozo ya usalama barabarani
- Kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya shule na taasisi husika pale linapotokea tatizo kwa gari la shule unaloendesha
- Kufuata mipangilio na ratiba za magari na maelekezo ya Dereva Mkuu kuhusu Route za magari
- Kushiriki sikukuu na shughuli za kijamii za The School of St. Jude mara zipangwapo
- Kutoa taarifa ya maandishi ikiwa gari unaloendesha litapata hitilafu au ajali itakayozuia safari iliyopangwa au ruti kuendelea.
Sifa za Mwombaji
- Awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 35
- Ajue kusoma na kuandika vizuri kwa Kiswahili. Kuzungumza, kuandika na/au kusoma kiingereza Itaboresha ombl
- Awe na leseni hal va udereva ya daraja "C-plain" na HGV "Class E" pamoja na vyeti vya madaraja hayo husika.
- Cheti cha Udereva kutoka kwenye chuo kinachotambulika
- Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) kuendesha mabasi ya shule pamoja na magari ya mizigo
Vigezo na Masharti Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu:
- Barva ya maombi iambatanishwe na
- Wasifu binafsi (CV)
- Barua ya uhakxi wa leseni kutoka polju.
- Nakale ya chell cha kuzaliwa
- Barue ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa anapoish
- Kuambatanisha cheti/nyaraka za kughushi itapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria
- Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Kampasi ya Moshong kabla ya tarehe 19/02/2026.
- Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.
TUTAWASILIANA NA WALE TU WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAJARIBIO NA MAHOJIANO!
ANGALIZO: TAFADHALI KUWA MAΚΙΝΙ ΝΑ ΜΑTENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI.
Fighting poverty through education PO Box 11875 Moshono, Arusha. Tanzania, East Africa +255 758 305776 +255 787 719 500 [email protected]
Interested in this job?
3 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
