Nafasi za Kazi 4 Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Job Role Insights
-
Date posted
2025-11-16
-
Closing date
2025-11-28
-
Hiring location
Kagera
-
Career level
Middle
-
Qualification
Bachelor Degree Certificate Degree Diploma High School Certificate Vocational / Technical
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
1 person
-
Gender
both
-
Job ID
125232
Job Description
The total number of job posts listed here for the Biharamulo District Council (Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo) is 4 posts in November 2025.
| Job Title | Posts |
| 1.0 Office Secretary Grade II (MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II) | 1 |
| 2.0 Driver Grade II (DEREVA DARAJA II) | 3 |
| TOTAL POSTS | 4 |
MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II
Nafasi: 1
Muda wa Maombi: 14/11/2025 - 28/11/2025
Majukumu na Wajibu
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Sifa za Mwombaji (Qualifications)
- Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six).
- Wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.
- Amepata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara (Remuneration)
- TGS.C
DEREVA DARAJA II
Nafasi: 3
Muda wa Maombi: 14/11/2025 - 28/11/2025
Majukumu na Wajibu
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji (Qualifications)
- Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara (Remuneration)
- TGS B
Interested in this job?
12 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
