Nafasi za Kazi 400 za Walimu wa Kujitolea (Mkataba) Tamisemi
Job Role Insights
-
Date posted
2026-06-02
-
Closing date
2026-06-14
-
Hiring location
Tanzania
-
Career level
Middle
-
Qualification
Advanced Degree Associate Degree Bachelor Degree Degree
-
Experience
2 Years
-
Quantity
1 person
-
Gender
both
-
Job ID
134660
Job Description
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TANGAZO LA NAFASI ZA WALIMU WA MKATABA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI KWA SOMO LA ELIMU YA BIASHARA
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushiriakiana na asasi ya Educate! Tanzania kupitia mradi wa kuboresha Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Elimu ya Biashara (Business Studies), inatekeleza afua ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Biashara (Business Studies).
Ofisi inatangaza nafasi 400 za walimu wa kujitolea (mkataba) wa somo la Elimu ya Biashara kwa ajili ya shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa, kwenye mikoa ifuatayo:
- Arusha
- Kilimanjaro
- Manyara
- Simiyu
- Kagera
- Geita
- Tabora
- Dodoma
- Morogoro
- Pwani
- Dar es Salaam
Lengo la mradi huu ni kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa wa Elimu ya Sekondari unaoelekeza ufundishwaji wa Somo la Elimu ya Biashara ili kuongeza ujuzi wa ujasiriamali kwa wanafunzi.
Hivyo, wahitimu wa Shahada (Degree) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kujitolea kufundisha Somo la Biashara katika shule za sekondari zitakazoorodheshwa kupitia Mfumo Rasmi wa Maombi ya ajira kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Muda wa kuwasilisha maombi:
- Kuanzia tarehe 1 Juni hadi 14 Juni, 2026
Walimu wa Kujitolea (mkataba) watakaokidhi vigezo watapangwa na kusimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
1.0 TARATIBU ZA KUOMBA
Waombaji wenye sifa wawasilishe maombi kupitia kiunganishi:
Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Biashara na Shahada ya Fani za Elimu ya Biashara au Uchumi (Degree in Business related fields or Economics) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0 SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI
Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
2.1 Shahada (Degree) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani hizi:
- Shahada ya Ualimu katika Masomo ya Biashara (Bachelor of Education in Business Studies / Business Education)
- Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce – BCom)
- Shahada ya Usimamizi wa Biashara (Bachelor of Business Administration – BBA)
- Shahada ya Uchumi au Shahada ya Sanaa katika Uchumi (Bachelor of Economics / Bachelor of Arts in Economics)
- Shahada katika Fani Nyingine Zinazohusiana na Masomo ya Biashara (Bachelor’s Degree in Other Business-Related Fields)
2.2 Masharti ya ziada:
- Taaluma ya msingi ya biashara, hata kama hana uzoefu wa kufundisha
- Uwezo wa kutumia kompyuta kwa shughuli za msingi za ufundishaji na ujifunzaji
3.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
Waombaji lazima wakidhi masharti yafuatayo:
- (i) Awe raia wa Tanzania
- (ii) Awe na umri usiozidi miaka 42
- (iii) Aambatishe nakala ya:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kidato cha Nne
- Kidato cha Sita (kama ipo)
- Fani ya Taaluma aliyosomea
- (iv) Awe tayari kufanya kazi katika shule zenye uhitaji mkubwa wa walimu
- (v) Hatabadilisha kituo au shule atakayopangiwa awali katika kipindi cha utekelezaji wa programu
- (vi) Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine
- (vii) Asiwe amewahi kufukuzwa au kustaafishwa kwa makosa ya kiutumishi
- (viii) Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- (ix) Waombaji waambatishe nyaraka zote muhimu katika mfumo
- (x) Waliosoma nje ya nchi:
- Wapata Namba ya Ulinganifu (EQ Number) kutoka NECTA
- (xi) Aambatishe barua ya maombi
MAWASILIANO
Kwa maelezo ya ziada wasiliana na TAMISEMI:
- Simu: 026 2160210 / 0735 160210
- Muda: 02:00 asubuhi – 10:00 jioni (siku za kazi)
MWISHO WA MAOMBI
- Tarehe: 14 Juni, 2026
- Saa: 05:59 usiku
Tangazo linapatikana pia:
TAMISEMI Official Website
Limetolewa na:
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
Mji wa Serikali – Mtumba
S.L.P 1923
41185 Dodoma
Interested in this job?
12 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
Generate Cover Letter
Login as a candidate to generate a free AI cover letter for this job
