Job Role Insights

  • Date posted

    2026-08-05

  • Closing date

    2026-08-17

  • Hiring location

    Zanzibar

  • Career level

    Middle

  • Experience

    1 - 2 Years

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    140268

Job Description

The total number of job posts listed here for the Zanzibar Examinations Council / Baraza la Mitihani la Zanzibar (Zanzibar Examinations Council - ZEC) is 2 posts in August 2026.

This specialized educational assessment software development recruitment targets full-stack systems engineering, database architecture, API integrations, and DevOps deployment in Unguja.

Job Title / SpecializationPosts
Afisa Msanifu Mifumo (System Developer 2) – Unguja2
TOTAL POSTS2

Baraza la Mitihani la Zanzibar (ZEC)

Vacancies: 2  |  Latest closing: Aug 17, 2026 Apply

AFISA MSANIFU MIFUMO (SYSTEM DEVELOPER 2)-UNGUJA

Posts: 2  |  Closing: Aug 17, 2026 Apply  |  Period: 04/08/2026 - 17/08/2026  |  Scale: ZPSH-01

Duties and Responsibilities

  • Kusanifu, kutengeneza, kufanya majaribio, kuweka katika matumizi (deploy System in to Production Development), kuendesha, na kutunza mifumo jumuishi ya TEHAMA (Full-Stack Applications), ikiwemo mifumo ya tovuti, programu za simu za mkononi, na mifumo ya kibiashara, kwa kuzingatia mahitaji ya Baraza, viwango vya ubora, usalama wa taarifa, na mbinu bora za uendelezaji wa programu.
  • Kujenga, kutekeleza na kuimarisha vipengele vya upande wa mtumiaji (Front-End) au upande wa seva (Back-End) kwa kutumia mifumo ya kisasa ya usanifu wa programu (Frameworks) na teknolojia zilizoidhinishwa.
  • Kusanifu, kutengeneza, kuimarisha utendaji na kusimamia hifadhidata (databases), hoja za hifadhidata (queries), taratibu zilizohifadhiwa (stored procedures), na miundo ya data (data models), kwa kuzingatia viwango vya ubora, usalama na ufanisi wa mifumo ya TEHAMA.
  • Kutengeneza, kutekeleza na kutunza miunganisho ya mifumo ya ndani na ya nje ya taasisi kwa kutumia Viunganishi vya Programu Tumizi (Application Programming Interfaces – APIs), Huduma za Tovuti (Web Services) na teknolojia nyingine za ujumuishaji wa mifumo (System Integration Technologies), ili kuhakikisha mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa kwa usalama.
  • Kuimarisha utendaji, usalama, uthabiti, upatikanaji (Availability) na uwezo wa mifumo kukuwa kulingana na mahitaji (scalability), pamoja na kutekeleza maboresho endelevu kwa kuzingatia Sera za Usalama wa Taarifa, Sera za TEHAMA, viwango vya ubora na miongozo ya Baraza la Mitihani la Zanzibar.
  • Kuchunguza, kubaini na kutatua hitilafu za mifumo katika mazingira ya uzalishaji (Production Environment), kurekebisha dosari za programu (Bugs), kuimarisha na kuhuisha mifumo, pamoja na kutoa msaada wa kiufundi ili kuhakikisha upatikanaji wa mifumo.
  • Kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na kazi yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake wa Kazi.

Qualifications

Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46.

Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya TEHAMA kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Awe na uwezo wa kutumia na kutengeneza mifumo ya komputa ya Taasisi kwa kutumia programing language kama TypeScript, Angular, React, Vue.js, Bootstrap, Tailwind CSS au PrimeNG, Spring Boot, Node.js (Express/NestJS), Laravel, (PHP), Python (Django), ASP.NET Core au Electron.

Uelewa mzuri wa mzunguko wa ujenzi wa programu (Software Development Life Cycle) na kufanya kazi katika mazingira yanayotumia mbinu ya Agile.

Ujuzi wa kutumia zana za maendeleo ya programu na DevOps, ikiwemo Git, GitHub au GitLab, pamoja na mifumo ya CI/CD kama GitHub Actions, GitLab CI au Jenkins. Uzoefu wa Docker na Kubernetes utakuwa sifa ya ziada.

Ujuzi wa kutengenezaji wa API, uthibitishaji wa watumiaji (JWT/OAuth2) na usanifu wa Microservices; uzoefu wa Full-Stack Development utakuwa sifa ya ziada.

Ujuzi wa kutumia angalau hifadhidata moja kati ya PostgreSQL, Microsoft SQL Server, Oracle Database au MongoDB.

Uwelewa wa matumizi ya programu huria (Open Source) itakuwa ni sifa ya ziada

Apply for this position

Interested in this job?

12 days left to apply

Apply now

Your job search, in your pocket

Get the ZoomTanzania Jobs app - apply on the go, get instant job alerts, and chat with our AI assistant anytime, anywhere.

How to Apply

Apply now