Nafasi za Kazi 9 Halmashauri ya Wilaya ya Songea November 2025
Job Role Insights
-
Date posted
2025-11-06
-
Closing date
2025-11-18
-
Hiring location
Ruvuma
-
Career level
Middle
-
Qualification
Bachelor Degree Certificate Degree Diploma
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
9 person
-
Gender
both
-
Job ID
124698
Job Description
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA
Kumb. Na. ΗΒ.9/364/01/3 05/11/2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Songea anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi tisa (09) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:
The Executive Director of the Songea District Council is advertising a total of nine (09) job vacancies. The positions open for application are Office Secretary Grade II (Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II) and Driver Grade II (Dereva Daraja II). Applications are invited from qualified Tanzanian citizens and must be submitted through the electronic recruitment portal no later than November 18, 2025.
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 04
1.1.1 ΚΑΖI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 MSHAHARA Cheo cha Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II kina ngazi ya mshahara wa TGS C
2.0 DEREVA DARAJA II - NAFASI 05
2.2.1 ΚΑZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa magari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
2.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI: Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha nne (Form IV) na leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.2.3 NGAZI YA MSHAHARA: Cheo cha Dereva II kina ngazi ya mshahara wa TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa sekretarieti ya ajirakatika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Diploma/Certificates,
- Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,
- Computer Certificate,
- Vyeti vya Kitaaluma.
- "Testmonial", "Provisional Results", "Statement of results", hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya udereva vilivyo wapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Novemba, 2025.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal').
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayata shughulikiwa.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani na barua hiyo ielekezwe kwa:
Barua ziandikwe kwa Anwani ifuatayo: -
- Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W)
- Halmashauri ya Wilaya ya Songea,
- 1 Barabara ya Halmashauri,
- S. L. P 995,
- 57183 SONGEA, RUVUMA
Imetolewa na: -
- MKURUGENZI MTENDAJI (W)
- SONGEA
Interested in this job?
12 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job
