Nafasi za Kazi za Kujitolea Kada ya Ualimu 1500 OWM-TAMISEMI

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-01-15

  • Closing date

    2026-01-28

  • Hiring location

    Tanzania

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Degree Diploma

  • Experience

    1 - 2 Years

  • Quantity

    10 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    126956

Job Description

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU (OWM-TAMISEMI)

TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI KUPITIA MRADI WA GPE - TSP

MAELEZO YA MRADI NA NAFASI

Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu "Global Partnership for Education Teacher Support Programme (GPE - TSP)" inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea. Kupitia mradi huu, OWM - TAMISEMI inatangaza nafasi za kujitolea kwa walimu 1,500 wa Shule za Sekondari zilizopo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye uhitaji mkubwa zaidi kwa kuzingatia utaratibu wa kupanga walimu wa Shule za Sekondari (Secondary Teacher Allocation Protocol - S-TAP). Nafasi hizi zinalenga walimu wa masomo ya Sayansi na Teknolojia (STEM), Masomo ya Amali (Vocational Subjects) na Masomo ya Biashara (Business Studies

The total number of volunteer job posts listed here for the President's Office - Regional Administration and Local Government (OWM-TAMISEMI) under the GPE Teacher Support Programme is 1,500 posts in January 2026.

Job TitlePosts
1.0 Volunteer Teacher - Physics (Mwalimu wa Kujitolea - Fizikia)504
2.0 Volunteer Teacher - Chemistry (Mwalimu wa Kujitolea - Kemia)246
3.0 Volunteer Teacher - Biology (Mwalimu wa Kujitolea - Biolojia)332
4.0 Volunteer Teacher - Mathematics (Mwalimu wa Kujitolea - Hisabati)418
TOTAL POSTS1,500

Majukumu ya Jumla ya Mwalimu wa Kujitolea

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi.
  • Kutengeneza na kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi.
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani.
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi kiakili, kimwili, kiroho na kutoa ushauri nasaha.
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya elimu.
  • Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za shule.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule.

Mchanganuo wa Nafasi na Sifa za Waombaji

Mwalimu wa Kujitolea - Somo la Fizikia (Nafasi 504)

  • Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) yenye somo la Fizikia; AU
  • Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la Fizikia; AU
  • Shahada isiyo ya Ualimu yenye somo la Fizikia + Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE); AU
  • Stashahada ya Ualimu (Diploma) yenye somo la Fizikia.

Mwalimu wa Kujitolea - Somo la Kemia (Nafasi 246)

  • Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) yenye somo la Kemia; AU
  • Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la Kemia; AU
  • Shahada isiyo ya Ualimu yenye somo la Kemia + Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE); AU
  • Stashahada ya Ualimu (Diploma) yenye somo la Kemia.

Mwalimu wa Kujitolea - Somo la Biolojia (Nafasi 332)

  • Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) yenye somo la Biolojia; AU
  • Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la Biolojia; AU
  • Shahada isiyo ya Ualimu yenye somo la Biolojia + Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE); AU
  • Stashahada ya Ualimu (Diploma) yenye somo la Biolojia.

Mwalimu wa Kujitolea - Somo la Hisabati (Nafasi 418)

  • Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) yenye somo la Hisabati; AU
  • Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la Hisabati; AU
  • Shahada isiyo ya Ualimu yenye somo la Hisabati + Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE); AU
  • Stashahada ya Ualimu (Diploma) yenye somo la Hisabati.

Masharti ya Jumla ya Waombaji

  • Awe raia wa Tanzania mwenye Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA).
  • Awe na umri usiozidi miaka 43.
  • Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu na taaluma.
  • Awe tayari kufanya kazi katika Shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa wa walimu.
  • Asiwe mwajiriwa wa Serikali au taasisi nyingine.
  • Awe hajawahi kufukuzwa au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa makosa ya kiutumishi.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi lazima wawe na Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) kutoka NECTA.

Jinsi ya Kutuma Maombi

  • Tovuti: Tembelea tovuti ya OWM - TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
  • Mfumo: Tumia kiunganishi cha Mfumo wa Ajira TAMISEMI (https://ajira.tamisemi.go.tz/).
  • Tarehe ya Maombi: Kuanzia tarehe 14 Januari 2026 hadi 28 Januari 2026.
  • Mwisho wa Kutuma: Tarehe 28 Januari 2026, saa 05:59 usiku.
  • Mawasiliano: Kituo cha huduma kwa wateja: 026 2160210 au 0735 160210.

Interested in this job?

13 days left to apply

Apply now

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

Apply now
Send message
Cancel