
Nafasi za Kazi za Muda INEC Kwaajili ya Uchaguzi Mkuu 2025
Job Role Insights
-
Date posted
2025-06-30
-
Closing date
2025-07-12
-
Hiring location
Tanzania
-
Career level
Middle
-
Qualification
Certificate O-Level Secondary Education Vocational / Technical
-
Experience
1 - 2 Years
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
Job Description
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025
Kwa madhumuni ya uendeshaji wa uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kikisomwa pamoja na kanuni ya 10(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 , Mkurugenzi wa Uchaguzi anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo:
- Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura.
- Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura.
- Makarani Waongozaji Wapiga Kura.
A. SIFA ZA WAOMBAJI WA NAFASI ZA WASIMAMIZI AU WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
- Awe raia wa Tanzania.
- Ametimiza umri wa miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu.
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (4) au zaidi na anajua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili au kiingereza.
- Pia, anayeweza kusoma na kuelewa kitabu cha Maelekezo kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura.
- Awe mkazi wa kata anayoomba kufanya kazi.
SIFA ZA WAOMBAJI WA NAFASI YA KARANI MWONGOZAJI WAPIGA KURA
- Awe raia wa Tanzania.
- Ametimiza umri wa miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu.
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (4) au zaidi na anajua kusoma na kuandika katika lugha ya kiswahili au kiingereza.
- Pia, anayeweza kusoma na kuelewa kitabu cha Maelekezo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura.
- Awe mkazi wa kata anayoomba kufanya kazi.
MALIPO
Malipo yatakuwa kama ifuatavyo:
- Siku ya Uchaguzi Msimamizi wa Kituo atalipwa posho ya Shilingi 70,000/= kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Shilingi 20,000/= kwa siku moja na nauli Shilingi 20,000/=.
- Msimamizi Msaidizi wa Kituo atalipwa posho ya Shilingi 65,000/= kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Shilingi 20,000/= kwa siku moja na nauli Shilingi 20,000/=.
- Karani Mwongozaji Wapiga Kura atalipwa posho ya Shilingi 65,000/= kwa siku moja na posho ya chakula Shilingi 20,000/=.
- Wakati wa mafunzo watendaji wote watalipwa posho ya kiasi cha Shilingi 50,000/= kwa siku na nauli kiasi cha Shillingi 20,000/= kwa kila siku ya mafunzo.
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji lazima aainishe kata na nafasi anayoomba.
- Mwombaji awe tayari kufanya kazi katika kituo chochote atakachopangiwa.
- Mwombaji aambatishe:
- Nakala ya vyeti vya Elimu ya Sekondari na Taaluma ikiwa anavyo.
- Wasifu (CV) ukionesha anuani yake ya makazi, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini wake wawili na namba zao za NIDA.
- Picha mbili zenye ukubwa sawa na picha iliyomo kwenye pasi ya kusafiria (Passport size) za hivi karibuni.
- Barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa serikali ya mtaa au kijiji katika eneo analoishi.
- Mwombaji ambaye ni mtumishi wa umma apitishe barua yake ya maombi kwa mwajiri wake.
E. NAMNA YA KUTUMA BARUA YA MAOMBI
- BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE ANUANI IFUATAYO:Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Uchaguzi House, Eneo la Uwekezaji Njedengwa, Kitalu D, Kiwanja Na.4, 5 Barabara ya Uchaguzi, S.L.P. 358, 41107 DODOMA.
- BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE NYUMA YA BAHASHA NAFASI ANAYOOMBA MWOMBAJI.
- ILI KURAHISISHA UTUMAJI WA MAOMBI, BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIKIWA ZIMEFUNGWA ZIPELEKWE KWA MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA AMBAYE ATAZIPOKEA NA KUZIWASILISHA KWA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI.
MWOMBAJI ATAKAYEBAINIKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KUGHUSHI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 11 JULAI, 2025
Limetolewa leo tarehe 28 Juni, 2025 na:
Kailima, R.K MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Interested in this job?
12 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job