Nafasi za Kazi The Lake Tanganyika Co-operative Union Ltd. (LATCU) Katavi

Job Role Insights

  • Date posted

    2025-09-02

  • Closing date

    2025-09-11

  • Hiring location

    Katavi

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree Degree Diploma

  • Experience

    1 - 2 Years

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    122658

Job Description

Chama cha Ushirika LATCU Ltd, ni chama kilichopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi kilichosajiliwa tarehe 11/11/1994 na kupata usajili wa Na. 5502, chama pia kilipata usajili mpya Namba AFF-KTV-MPN-MC-2023-93 mnamo tarehe 16/02/2023. Ambapo kilianzishwa kwa misingi ya kuwasaidia wakulima wa mazao mchanganyiko kupata pembejeo na masoko na bei za mazao, ugani uwakilishi katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa. Uongozi wa Bodi ya LATCU Ltd wanatarajia kuajiri watu wenye sifa na uwezo ili kujaza nafasi zilizo wazi.

AFISA UGANI NAFASI MBILI (2)

1.1. Majukumu ya kazi

  • Kufundisha wakulima matumizi sahihi ya pembejeo.
  • Kuelimisha wakulima kupata mazao bora na yenye tija.
  • Kuandaa mpango kazi wa mwaka wa Idara.
  • Kufanya kazi zingine zinazohusiana na madhumuni ya kuanzishwa kwa LATCU Ltd.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe ni Mtanzania.
  • Awe na stashahada ya kilimo kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Awe angalau na uzoefu wa kazi kuanzia mwaka mmoja na kama Afisa Ugani.
  • Awe na uwezo wa kuelimisha mkulima awapo shambani.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Awe na Leseni/ujuzi wa kuendesha pikipiki.
  • Awe na umri kuanzia miaka 18-45.
  • Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa Lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

KATIBU MUHTASI NAFASI MOJA (1)

2.1. Majukumu ya kazi

  • Kuchapa barua/taarifa na nyaraka za kawaida.
  • Kupokea na kutuma barua pepe (Email za kiofisi kwa ofisi anayehusika kwa wakati.
  • Kuandaa safari za kikazi pamoja na nyaraka hitajika za Meneja Mkuu.
  • Kusaidia kupokea wageni, kuwasilisha shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza.
  • Kusaidia kutunza taarifa/kupatiwa huduma za kumbukumbu za matukio, mihadi, wageni tarehe za vikao, safari za mkuu wake wa kazi na ratiba za kazi nyingine.
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi kwa wasaidizi wake ofisini.
  • Kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake.
  • Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na viongozi wake.

2.2. SIFA YA MWOMBAJI

  • Awe ni Mtanzania.
  • Mwombaji awe na elimu ya stashahada ya mafunzo ya Chuo cha Uhazili au kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe angalau na uzoefu wa mwaka mmoja kama Katibu Muhtasi.
  • Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Umri kuanzia miaka 18-45.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

LATCU Ltd inatoa haki sawa kwa watu wote wenye sifa katika masuala ya Ajira.

  • Mwombaji anaweza kuwasilisha barua aliyoandika kwa mkono au kuchapishwa ikiwa imesainiwa.
  • Maombi yaambatanishwe na Nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria au mahakama.
  • Wasifu (CV) uliosainiwa na mwombaji.
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Nakala ya cheti cha kuhitimu kidato cha nne na cha sita, na Nakala ya vyeti vya Taaluma na matokeo ya mitihani kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika na Serikali.
  • Picha mbili (2) za "passport size" za hivi karibuni.
  • Mwombaji aambatanishe Nakala ya vyeti vyake na namba ya simu ya mkononi au ya watu wake wa karibu katika mawasiliano yake, na anuani ya barua pepe (Email Adress).
  • Mawasiliano hayo muhimu katika kuwaita wahusika kwenye usaili.
  • Muombaji aliyejitolea/Kufanya kazi kwenye taasisi yoyote ile inayotambulika Tanzania atapewa kipaumbele.
  • Barua na viambata vitakavyowekwa kwa barua pepe (Email), kwa watakaofanikiwa kuitwa kwenye usaili wawe na Nakala halisi (Originals).
  • Barua za maombi zitumwe kwa anuani ifuatavyo:
    • MENEJA MKUU,
    • LAKE TANGANYIKA CO-OPERATIVE UNION (LATCU) LIMITED
    • S.L.P. 251,
    • MPANDA-KATAVI
    • Email: [email protected]

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10/09/2025 saa 10:00 jioni.

Interested in this job?

9 days left to apply

Apply now

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

LATCU Ltd inatoa haki sawa kwa watu wote wenye sifa katika masuala ya Ajira. Mwombaji anaweza kuwasilisha barua aliyoandika kwa mkono au kuchapishwa ikiwa imesainiwa. Maombi yaambatanishwe na Nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria au mahakama. Wasifu (CV) uliosainiwa na mwombaji. Nakala ya cheti cha kuzaliwa. Nakala ya cheti cha kuhitimu kidato cha nne na cha sita, na Nakala ya vyeti vya Taaluma na matokeo ya mitihani kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika na Serikali. Picha mbili (2) za "passport size" za hivi karibuni. Mwombaji aambatanishe Nakala ya vyeti vyake na namba ya simu ya mkononi au ya watu wake wa karibu katika mawasiliano yake, na anuani ya barua pepe (Email Adress). Mawasiliano hayo muhimu katika kuwaita wahusika kwenye usaili. Muombaji aliyejitolea/Kufanya kazi kwenye taasisi yoyote ile inayotambulika Tanzania atapewa kipaumbele. Barua na viambata vitakavyowekwa kwa barua pepe (Email), kwa watakaofanikiwa kuitwa kwenye usaili wawe na Nakala halisi (Originals). Barua za maombi zitumwe kwa anuani ifuatavyo: MENEJA MKUU, LAKE TANGANYIKA CO-OPERATIVE UNION (LATCU) LIMITED S.L.P. 251, MPANDA-KATAVI Email: [email protected]

Apply now
Whatsapp-color Created with Sketch. Job Alert
Subscribe to receive instant alerts of new relevant jobs directly to your WhatsApp.
Subcrible
Send message
Cancel