Kuitwa Kwenye Usaili TANESCO na MDAs & LGAs
Notice details
-
Date posted
2026-11-23
-
Interview date
2026-12-15
-
Venue
Tanzania
-
Notice ID
152804
About this notice
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya MDAs & LGAs, Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) na Halmashauri ya Wilaya ya Siha, anapenda kuwataarifu waombaji wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28/11/2026 hadi 15/12/2026. Baada ya kukamilika kwa usaili, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe zilizoainishwa katika tangazo hili. Muda na maeneo ya kufanyia usaili vimeainishwa kwa kila kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika katika eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (mask).
- Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Mkazi.
- Kitambulisho cha Mpiga Kura.
- Kitambulisho cha Kazi.
- Kitambulisho cha Uraia.
- Hati ya Kusafiria.
- Leseni ya Udereva.
- Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au Kijiji anachotoka.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Kidato cha Nne na Sita, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea, kutegemeana na sifa za nafasi husika.
- Wasailiwa watakaowasilisha nyaraka za Testimonials, Provisional Results, Statement of Results au hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI Results Slips) HAWATAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
- Kwa kada zinazohitaji usajili katika Bodi za Kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kufika na vyeti vyao HALISI vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.
- Kila msailiwa atajigharamia mwenyewe kwa chakula, usafiri na malazi. Aidha, kila msailiwa anapaswa kuhudhuria usaili akiwa amevaa mavazi nadhifu na yenye staha, kwa kuzingatia Waraka wa Mavazi.
- Wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha kuwa vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika, kama vile TCU, NACTVET au NECTA. Aidha, wasailiwa wa kada zinazohitaji GPA ambao wamesoma nje ya Tanzania wanapaswa kuwasilisha cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
- Wasailiwa ambao hawajaona majina yao katika tangazo hili wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kuona sababu za kutokuitwa kwenye usaili, kwa lengo la kuepuka kukosa fursa zinazoweza kujitokeza wakati mwingine.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuhakikisha wanaingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kunakili namba zao za usaili. Aidha, wasailiwa watakaofanya usaili wa mchujo kwa njia ya mtandao wanapaswa kukumbuka anuani zao za barua pepe (email address) na nywila (password) wanazotumia kuingia kwenye mfumo wa Ajira Portal.
- Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
- Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki zilizoainishwa katika tangazo husika la kazi pamoja na muundo wa utumishi wa idara inayohusika.
