He

About me

Mtaalamu wa Benki na Fedha mwenye shahada ya kwanza katika Usimamizi wa Benki na Fedha, mwenye uzoefu katika shughuli za mikopo, tathmini ya uwezo wa wateja kukopa, huduma kwa wateja na ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo. Kwa sasa nafanya kazi kama Afisa Mikopo katika SLS Microfinance Ltd, nikiwa na uwezo wa kusimamia mikopo, kufuatilia marejesho, kutunza kumbukumbu sahihi za kifedha na kujenga mahusiano mazuri na wateja. Nina ujuzi mzuri wa mawasiliano, uchambuzi, utatuzi wa changamoto na usimamizi wa mahusiano na wateja. Nimejizatiti kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kwa kuzingatia malengo ya taasisi ili kuchangia ukuaji na mafanikio ya taasisi.