Kuitwa Kazini Taasisi za Umma 19-01-2026 (Usaili Uliofanyika 16-01-2025 na 22-12-2025)

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-01-20

  • Closing date

    2026-02-02

  • Hiring location

    Tanzania

  • Quantity

    10 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    127038

Job Description

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na. JA. 9/ 18/01" D"/90 Tarehe: 19/01/2026

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 16-01-2025 na tarehe 22-12-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Maelekezo Muhimu kwa Waliofaulu

  • Upatikanaji wa Barua: Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata BARUA zao kupitia akaunti zao za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications. Wanapaswa kupakua na kutoa nakala (Download and Print) barua hizo kwa ajili ya kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
  • Utaratibu wa Kuripoti: Waliofaulu wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri katika muda uliopangwa na ulioainishwa ndani ya barua zao za kupangiwa kituo cha kazi.
  • Uhakiki wa Vyeti: Ni sharti kufika na vyeti halisi (Original Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kukabidhiwa barua rasmi ya ajira.

Ujumbe kwa Ambao Majina Hayapo

  • Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili kwa wakati huu. Wanahimizwa wasisite kuomba tena nafasi nyingine za kazi zitakapotangazwa hapo baadaye.

View the full list here

13 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel