Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) 25/01/2026
Job Role Insights
-
Date posted
2026-01-26
-
Closing date
2026-02-15
-
Hiring location
Tanzania
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
127240
Job Description
KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA
Kumb. Na: CAC.29/86/01/B/58 Tarehe: 25 Januari, 2026
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Kampuni ya Ndege Tanzania inapenda kuwataarifu wote walioomba kazi katika kada mbalimbali kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 31 Januari, 2026 hadi tarehe 6 Februari, 2026.
RATIBA YA USAILI
- Usaili wa Mchujo: Utafanyika tarehe 31 Januari, 2026.
- Usaili wa Mahojiano: Utafanyika kuanzia tarehe 3 Februari hadi 6 Februari 2026.
- Muda na Mahali: Maelezo ya muda na sehemu ambapo usaili utafanyika yameainishwa kwenye orodha ya majina (katika tangazo kamili).
MAAGIZO MUHIMU KWA WASAILIWA
- Vitambulisho: Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria, au Leseni ya Udereva.
- Vyeti Halisi (Originals): Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha Nne, Sita, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, na Shahada kulingana na sifa za mwombaji.
- Nyaraka Zisizokubalika: "Testimonials", "Provisional Results", "Statement of Results", na Hati za Matokeo (Result Slips) za Kidato cha Nne na Sita HAZITAKUBALIWA na wahusika hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
- Gharama: Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi.
- Uzingatiaji wa Ratiba: Kila msailiwa azingatie tarehe, muda, na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Tofauti ya Majina: Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika vyeti vya elimu, taaluma, na cheti cha kuzaliwa wahakikishe wanakuwa na Kiapo cha Kubadilisha Majina kilichosajiliwa (DEED POLL).
- Waliozaliwa Nje ya Nchi: Wasailiwa waliozaliwa nje ya Tanzania wahakikishe wanawasilisha uthibitisho wa uraia kutoka Ofisi za Uhamiaji.
- Wasioitwa: Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
View the full list here
This job has expired
