Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kuanzia Tarehe 14/02/2026

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-02-04

  • Closing date

    2026-02-14

  • Hiring location

    Tanzania

  • Quantity

    10 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    127515

Job Description

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Kumb. Na: JA.9/16/01/8 Tarehe: 03/02/2026

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya MDAs & LGAs, anawataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14/02/2026 hadi 14/02/2026.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

  1. Muda na Mahali: Usaili utafanyika kuanzia tarehe, muda, na sehemu iliyoainishwa kwa kila Kada kwenye tangazo hili.
  2. Barakoa: Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
  3. Kitambulisho: Kila msailiwa lazima awe na kitambulisho kinachokubalika (Kitambulisho cha Mkazi, Mpiga Kura, Kazi, Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji).
  4. Vyeti Halisi: Lazima kufika na VYETI VYAO HALISI (Cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, nk).
  5. Nyaraka Zisizokubalika: ‘Testimonials’, ‘Provisional Results’, ‘Statement of Results’, na hati za matokeo za ‘result slips’ (Kidato cha IV na VI) HAVITAKUBALIWA na wahusika hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
  6. Usajili wa Kitaaluma: Kwa kada zinazohitaji kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma, ni lazima kuja na Vyeti Halisi vya Usajili na Leseni za kufanyia kazi.
  7. Gharama na Mavazi: Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri, na Malazi. Mavazi lazima yawe nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
  8. Vyeti vya Nje ya Nchi: Waliosoma nje ya Tanzania lazima vyeti vyao viwe vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET, au NECTA). Kwa kada zinazohitaji GPA, lazima kuwasilisha cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
  9. Majina Ambayo Hayaonekani: Wasailiwa wasioona majina yao waingie kwenye akaunti zao za ‘Ajira Portal’ ili kuona sababu za kutokuitwa.
  10. Ajira Portal & Namba ya Usaili: Wasailiwa walioitwa wahakikishe wanakili namba ya usaili kutoka kwenye akaunti zao. Kwa usaili wa mchujo wa mtandao, kumbuka barua pepe na nywila (password) za Ajira Portal.
  11. Tofauti ya Majina: Ikiwa majina yanatofautiana kwenye nyaraka, lazima kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

View the full list here

8 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel