Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs Kuanzia Tarehe 14/02/2026
Job Role Insights
-
Date posted
2026-02-04
-
Closing date
2026-02-14
-
Hiring location
Tanzania
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
127515
Job Description
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Kumb. Na: JA.9/16/01/8 Tarehe: 03/02/2026
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya MDAs & LGAs, anawataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14/02/2026 hadi 14/02/2026.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
- Muda na Mahali: Usaili utafanyika kuanzia tarehe, muda, na sehemu iliyoainishwa kwa kila Kada kwenye tangazo hili.
- Barakoa: Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
- Kitambulisho: Kila msailiwa lazima awe na kitambulisho kinachokubalika (Kitambulisho cha Mkazi, Mpiga Kura, Kazi, Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji).
- Vyeti Halisi: Lazima kufika na VYETI VYAO HALISI (Cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, nk).
- Nyaraka Zisizokubalika: ‘Testimonials’, ‘Provisional Results’, ‘Statement of Results’, na hati za matokeo za ‘result slips’ (Kidato cha IV na VI) HAVITAKUBALIWA na wahusika hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
- Usajili wa Kitaaluma: Kwa kada zinazohitaji kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma, ni lazima kuja na Vyeti Halisi vya Usajili na Leseni za kufanyia kazi.
- Gharama na Mavazi: Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri, na Malazi. Mavazi lazima yawe nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
- Vyeti vya Nje ya Nchi: Waliosoma nje ya Tanzania lazima vyeti vyao viwe vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET, au NECTA). Kwa kada zinazohitaji GPA, lazima kuwasilisha cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
- Majina Ambayo Hayaonekani: Wasailiwa wasioona majina yao waingie kwenye akaunti zao za ‘Ajira Portal’ ili kuona sababu za kutokuitwa.
- Ajira Portal & Namba ya Usaili: Wasailiwa walioitwa wahakikishe wanakili namba ya usaili kutoka kwenye akaunti zao. Kwa usaili wa mchujo wa mtandao, kumbuka barua pepe na nywila (password) za Ajira Portal.
- Tofauti ya Majina: Ikiwa majina yanatofautiana kwenye nyaraka, lazima kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
View the full list here
8 days left to report
Share this opportunity
Help others find their dream job
