Tangazo la Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali za Umma 09-01-2026

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-01-10

  • Closing date

    2026-01-23

  • Hiring location

    Tanzania

  • Gender

    both

  • Job ID

    126763

Job Description

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 11-01-2025 na tarehe 28-11-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

MAAGIZO KWA WALIOFAULU

Jinsi ya Kupata Barua:

Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, barua zao za kupangiwa vituo vya kazi watazipata kupitia akaunti zao za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications. Hivyo, watapaswa kupakua na kutoa nakala (Download and Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.

Utaratibu wa Kuripoti na Vyeti:

Waombaji kazi walio faulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.

UJUMBE KWA AMBAO MAJINA HAYAKUTOKA

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi au hawa kufaulu usaili. Hivyo, wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapo tangazwa.

View the full list here

11 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel