Tangazo la Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali za Umma 11-01-2026
Job Role Insights
-
Date posted
2026-01-12
-
Closing date
2026-01-25
-
Hiring location
Tanzania
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
126828
Job Description
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 14-01-2025 na tarehe 22-12-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
MAAGIZO KWA WALIOFAULU
Upatikanaji wa Barua: Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, barua zao zinapatikana kupitia akaunti zao za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications. Waombaji wanapaswa kupakua na kutoa nakala (Download and Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Kuripoti na Uhakiki wa Vyeti: Waombaji kazi waliofaulu wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ulioainishwa kwenye barua zao. Ni lazima wafike wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi ya Ajira.
UJUMBE KWA AMBAO MAJINA HAYAKUTOKA
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili. Hivyo, wanashauriwa wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapo tangazwa.
View the full list here
13 days left to report
Share this opportunity
Help others find their dream job
