Tangazo la Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali za Umma 23-12-2025
Job Role Insights
-
Date posted
2025-12-24
-
Closing date
2026-01-06
-
Hiring location
Tanzania
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
126434
Job Description
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anatoa taarifa kwa waombaji kazi waliofanya usaili kati ya tarehe 23-04-2025 na tarehe 19-11-2025 kuhusu matokeo ya usaili na upangaji wa vituo vya kazi.
MATOKEO YA USAILI NA UPANGAJI WA VITUO
Matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
UTARATIBU WA KUPATA BARUA ZA KUPANGIWA KAZI
Wasailiwa wote waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi watazipata barua zao kupitia AKAUNTI zao za Ajira Portal.
- Mtumiaji anapaswa kuingia kwenye akaunti yake na kwenda sehemu ya My Applications.
- Ni lazima kupakua na kutoa nakala (Download and Print) ya barua hizo.
- Barua hizo ndizo zitakazotumika kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
MAHITAJI NA MUDA WA KURIPOTI
Waombaji waliofaulu wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao. Wakati wa kuripoti, mhusika anapaswa kuwa na:
- Vyeti halisi (Original Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
- Vyeti hivi vitahakikiwa na mwajiri kabla ya mhusika kupewa barua ya Ajira.
TAARIFA KWA WALE AMBAO HAWAJAFAULU
Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili kwa wakati huu. Sekretarieti inawahimiza wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa hapo baadaye.
View the full list here
13 days left to report
Share this opportunity
Help others find their dream job
