Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Ofisi ya Bunge Majina ya Nyongeza 20-12-2025

Job Role Insights

  • Date posted

    2025-12-20

  • Closing date

    2025-12-23

  • Hiring location

    Tanzania

  • Gender

    both

  • Job ID

    126364

Job Description

Katibu wa Bunge Ofisi ya Bunge anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 20/12/2025 hadi 23/12/2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili
    utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
    Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,
    Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya
    utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji anachotoka.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada,
    Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za nafasi husika.
  • Wasailiwa watakaowasilisha ‘Testimonials, Provisional Results, Statement of results’, hati za matokeo za kidato
    cha IV na VI (‘form IV and form VI results slips’) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA
    USAILI.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili
    pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi. Aidha kila msailiwa anapaswa kuhudhuria usaili akiwa
    na mavazi nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
  • Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka
    husika (kama TCU, NACTVET au NECTA). Wasailiwa wa kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania
    wawasilishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
  • Wasailiwa ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za ‘Ajira
    Portal’ na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili.
    Aidha wasailiwa watakaofanya usaili wa mchujo kwa njia ya Mtandao wanapaswa kukumbuka barua pepe (email
    address) na nywila (password) zao wanazotumia katika mfumo wa Ajira Portal.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha
    Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

View the full list here

1 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel