Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Taasisi Mbalimbali za Umma 08-01-2026

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-01-10

  • Closing date

    2026-01-18

  • Hiring location

    Tanzania

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    126766

Job Description

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi katika taasisi mbalimbali zikiwemo Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO), MDAs & LGAs, RUWASA, Makumbusho ya Taifa (NMT), Tume ya Madini (TMC), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), VETA, TEMESA, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), TIRDO, CAMARTEC, NAOT, na NHC kuwa usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 18/01/2026 hadi 14/02/2026.

MAAGIZO MUHIMU KWA WASAILIWA

  • Ratiba ya Usaili: Usaili utafanyika kulingana na tarehe, muda, na mahali palipoainishwa kwa kila kada kwenye tangazo husika.
  • Barakoa: Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (Mask).

Vitambulisho: Wasailiwa lazima wawe na vitambulisho vya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni Kitambulisho cha Mkazi, Mpiga kura, Kazi, Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva, au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji.
Vyeti Halisi (Originals): Ni lazima kufika na vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne, Sita, Astashahada, Stashahada, na Shahada kulingana na sifa za nafasi.
Nyaraka Zisizokubalika: 'Testimonials', 'Provisional Results', 'Statement of Results', na hati za matokeo (results slips) za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa na mhusika hataruhusiwa kuendelea na usaili.

  • Usajili wa Kitaaluma: Kwa kada zinazohitaji kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma, waombaji wanapaswa kuja na vyeti halisi vya usajili pamoja na leseni za kazi.
  • Gharama na Mavazi: Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi. Pia, lazima kuhudhuria usaili na mavazi nadhifu na yenye staha.
  • Vyeti vya Nje ya Nchi: Waliosoma nje ya Tanzania lazima wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na TCU, NACTVET, au NECTA. Cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU kinahitajika kwa kada zinazohitaji GPA.
  • Kutoitwa Kwenye Usaili: Waombaji ambao majina yao hayapo wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za 'Ajira Portal' ili kuona sababu za kutokuitwa.

Akaunti ya Ajira Portal: Wasailiwa wanakumbushwa kuingia kwenye akaunti zao kunakili namba ya usaili na kuhakikisha wanakumbuka barua pepe na nywila (password) zao, hasa kwa usaili wa mchujo wa mtandao.
Tofauti ya Majina: Ikiwa majina yanatofautiana kwenye nyaraka, msailiwa anapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

View the full list here

6 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel