Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Wizara ya Maliasili na Utalii Ajira za Mkataba 05-01-2026

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-01-05

  • Closing date

    2026-01-18

  • Hiring location

    Tanzania

  • Gender

    both

  • Job ID

    126533

Job Description

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi za Sustainable Food Systems Specialist in the Rice Sector Development na Gender and Safe Guard Specialist katika mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi na Urejeshaji wa Mandhari katika Maeneo ya Misitu ya Tanzania (FOLUR). Mradi huu unatekelezwa na Wizara kama Wakala Mkuu wa Utekelezaji kwa ushirikiano na Shirika la World Wildlife Fund (WWF), ambapo usaili unatarajiwa kufanyika tarehe 09-01-2026.

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe iliyooneshwa kwenye tangazo hili huku muda na sehemu husika vikiwa vimeainishwa kwa kila mhusika.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (mask) kwa ajili ya usalama wa afya.
  • Ni lazima kwa kila msailiwa kuwa na kitambulisho cha utambuzi, ambapo vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na Kitambulisho cha NIDA, Mpiga kura, Kazi, Mkaazi, au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne, kidato cha sita, stashahada, na shahada kulingana na sifa za mwombaji.
  • Nyaraka kama Testimonials, Provisional Results, Statement of results, au hati za matokeo za kidato cha nne na sita hazitakubaliwa na mhusika hataruhusiwa kuendelea na usaili.
  • Kila msailiwa atajigharamia mwenyewe kwa chakula, usafiri, na malazi wakati wote wa mchakato wa usaili.
  • Ni muhimu kwa kila msailiwa kuzingatia kwa ukamilifu tarehe, muda, na mahali mahususi alipopangiwa kufanyia usaili wake.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE, au NECTA.
  • Wale ambao majina yao hayakuonekana kwenye tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo na wasisite kuomba tena pindi nafasi nyingine zitakapotangazwa.
  • Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuwasilisha vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni hai za kufanyia kazi kutoka kwenye bodi zao.

View the full list here

6 days left to report

View Names

Share this opportunity

Help others find their dream job

How to Apply

View Names
Send message
Cancel