Re-Advertised: Meneja (Nafasi 1) Bodi ya DUWASA Saccos Ltd

by DUWASA Saccos Ltd in
812 (views)

Job Role Insights

  • Date posted

    2026-06-30

  • Closing date

    2026-07-15

  • Hiring location

    Dodoma

  • Career level

    Middle

  • Qualification

    Bachelor Degree

  • Experience

    3 - 5 Years

  • Quantity

    1 person

  • Gender

    both

  • Job ID

    131530

Job Description

DUWASA Saving and Credit Co-operative Society (DUWASA SACCOS) ni ushirika wa akiba na mikopo uliopo jijini Dodoma ulioanzishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003 na kurekebishwa mwaka 2013. SACCOS hii imeundwa na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa lengo la kuinua hali ya kiuchumi ya wanachama wake kupitia huduma bora za kifedha, mikopo nafuu, na elimu ya uwekezaji.

Bodi ya DUWASA SACCOS Ltd inakusudia kuajiri Meneja mwenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa kutosha katika kusimamia na kuendesha shughuli za ushirika wa akiba na mikopo. Meneja/Katibu wa chama atakuwa msimamizi wa shughuli zote za kila siku za chama kulingana na miongozo iliyopo na maelekezo yatakayotolewa na Bodi.

Elimu na Ujuzi

  • Awe na Shahada ya Usimamizi wa Biashara, Uhasibu, Fedha au Uchumi kutoka katika chuo kinachotambulika na kusajiliwa na Serikali.
  • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3).
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
  • Awe na uwezo wa kujituma na kufanya kazi bila kutegemea mtu mwingine.
  • Awe mbunifu katika uendelezaji wa shughuli za chama.
  • Awe na uwezo wa kuandaa hesabu za chama na kuziwasilisha kwenye Bodi ya Chama, wanachama na wadau wengine.

Majukumu ya Nafasi ya Meneja

  • Kusimamia shughuli zote za kiutendaji na fedha za SACCOS.
  • Kuandaa na kutekeleza mipango mkakati na bajeti ya mwaka.
  • Kuhakikisha utunzaji sahihi wa kumbukumbu za fedha na wanachama.
  • Kuandaa taarifa za fedha za kila mwezi na mwaka.
  • Kusimamia ukusanyaji wa madeni na kuzuia limbikizo la mikopo.
  • Kuwa kiungo kati ya Bodi ya Wakurugenzi, wanachama na mamlaka za udhibiti.

Mambo ya Kuzingatia kwa Mwombaji

  • Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Ambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Ambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani, namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita (kwa waliofikia kiwango hicho), pamoja na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ngazi mbalimbali kulingana na sifa za kazi hii.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, na Form IV/Form VI Results Slips havitakubaliwa.
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayatafikiriwa.
  • Ambatanisha barua ya maombi iliyosainiwa na kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma barua ya maombi, wasifu (CV), na nakala za vyeti vya taaluma kwa:

Mwenyekiti wa Bodi
Chama cha Akiba na Mikopo DUWASA SACCOS Ltd
Barabara ya Mkapa
S.L.P. 431
Dodoma

Barua pepe: [email protected]

Mwisho wa Kutuma Maombi

Jumatano, tarehe 15 Julai 2026, saa 5:59 usiku.e: [email protected]

Mwisho wa Kutuma Maombi

15 Julai 2026 saa 5:59 usiku.

Interested in this job?

This job has expired

Apply now

Your job search, in your pocket

Get the ZoomTanzania Jobs app - apply on the go, get instant job alerts, and chat with our AI assistant anytime, anywhere.

How to Apply

MWENYEKITI WA BODI CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPО, DUWASA BARABARA YA MKAPA, SLP 431 DODOMA Barua pepe: [email protected] Imetolewa leo tarehe 03/05/2026 DUWASA SACCOS LTD

Apply now