Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama
Job Role Insights
-
Date posted
2025-12-12
-
Closing date
2025-12-25
-
Hiring location
Tanzania
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
-
Job ID
126186
Job Description
Kufuatia tangazo la nafasi za ajira mpya zilizotangazwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama tarehe 17 Novemba, 2025, taarifa ifuatayo inatolewa kwa waombaji waliochaguliwa kuingia kwenye usaili wa hatua ya kwanza:
HATUA YA KWANZA YA USAILI
- Aina ya Usaili: Usaili utafanyika kwa njia ya Kielektroniki kwa kila Kada iliyoainishwa kwenye jedwali.
- Tarehe na Muda: Usaili utaanza kuanzia Saa 2:30 Asubuhi kwa tarehe, muda na vituo vilivyooneshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa iliyoambatishwa na Tangazo hili.
- Mahali: Wasailiwa watafanya usaili kwenye vituo walivyopangiwa vilivyooneshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa.
NYARAKA MUHIMU ZA KUFIKA NAVYO
Wasailiwa wote wafike na nyaraka zifuatazo halisi:
- Vyeti vya Elimu.
- Vyeti vya Taaluma.
- Vyeti vya kuzaliwa.
- Kitambulisho chenye picha kinachotambulika na Serikali.
TAHADHARI NA VIGEZO
- Wasailiwa hawatasailiwa ikiwa watafika kwenye vituo vya usaili bila kuwa na nyaraka zilizoainishwa.
- Wasailiwa hawatasailiwa ikiwa watafika nje ya muda wa usaili uliopangwa.
- Wale ambao hawataona majina yao kwenye tovuti, watambue kuwa hawakupata nafasi ya kufanya usaili.
- Wasailiwa wote wazingatie kuhudhuria usaili kwenye vituo walivyopangiwa.
HATUA INAYOFUATA
- Wasailiwa watakaofaulu usaili katika hatua ya kwanza watafahamishwa tarehe ya hatua nyingine ya usaili wa kujieleza (Oral Interview) na/au vitendo (Practical interview).
- Taarifa kuhusu hatua zinazofuata zitatolewa kupitia tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama (www.jsc.go.tz).
MAWASILIANO KWA MAULIZO
- Simu: 0734219821 au 0738247341
- Barua pepe: [email protected]
- Imetolewa na: Tume ya Utumishi wa Mahakama.
View the full list here
13 days left to report
Share this opportunity
Help others find their dream job
