Tangazo la Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali za Umma
Notice details
-
Date posted
2026-11-24
-
Reporting date
2026-11-30
-
Venue
Tanzania
-
Notice ID
152871
About this notice
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 17/12/2025 na tarehe 11/11/2026 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina iliyotolewa pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi kufuatia kupatikana kwa nafasi za kazi.
Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata barua zao za kupangiwa vituo vya kazi kupitia akaunti zao za Ajira Portal, katika sehemu ya My Applications. Hivyo, wanatakiwa kupakua na kuchapisha (Download and Print) barua hizo na kwenda nazo wanaporipoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kwa waajiri wao ndani ya muda ulioainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi. Wanaporipoti, wanapaswa kuwa na vyeti vyao halisi vya elimu, kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea, kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi ya ajira.
Waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili wanapaswa kutambua kuwa hawakufaulu usaili au hawakupata nafasi za kazi zilizotangazwa. Hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
The Secretary of the Public Service Recruitment Secretariat wishes to inform applicants who applied for various positions and attended interviews conducted between 17 December 2025 and 11 November 2026 that the list of successful candidates is as published in this announcement.
The list also includes some candidates who were previously placed in the database for various cadres and have now been allocated workstations following the availability of vacancies.
All candidates who passed the interviews and have been allocated workstations will receive their appointment allocation letters through their Ajira Portal accounts under the My Applications section. Candidates are required to download and print these letters and present them when reporting to their respective assigned workstations.
Furthermore, successful candidates who have been allocated workstations are required to report to their respective employers within the period specified in their allocation letters. Upon reporting, they must bring their original academic certificates, starting from the Certificate of Secondary Education Examination (Form Four) and above, for verification by the employer before being issued with their official employment letters.
Applicants whose names do not appear in this announcement should understand that they were not successful in the interviews or were not selected for the available positions. They are encouraged to apply again when new job vacancies are advertised.
